Soul Boy

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Soul Boy[1] ni filamu ya Kenya iliyoandikiwa na Billy Kahora na kuongozwa na Hawa Essuman. Ilikuwa chini ya Tom Tykwer ambaye ni muongozaji na mtayarishaji wa filamu kutoka Ujerumani huko Kibera, moja ya makazi duni katika bara la Afrika, katikati mwa jiji la Nairobi, Kenya. Filamu ilipata uteuzi mara tano mwaka 2007 katika tuzo za African Movie Academy Awards.[2] Filamu hii ilitoka katika karakana ya vijana wapenda filamu jijini Nairobi, ikiongozwa na muongozaji Tom Tykwer kutoka ujerumani.

Kisa cha filamu[hariri | hariri chanzo]

Abila mwenye umri wa miaka 14 anaishi Nairobi, Kenya na wazazi wake huko Kibera, moja ya makazi duni zaidi katika Afrika Mashariki. Asubuhi moja kijana uyu anagundua baba yake ni mwenye huzuni na pia mgonjwa. Kuna mtu ameiba roho yake, baba ananung'unika. Abila anachanganyikiwa na kupata mshituko lakini anataka kumsaidia baba yake kutafuta tiba sahihi. Akiungwa mkono na mpenzi wake Shiku, anaanza safari ya kusisimua inayompeleka hadi kwenye chimbuko lake.

Wahusika[hariri | hariri chanzo]

  • Samson Odhiambo
  • Leila Dayan Opou
  • Krysteen Savane
  • Frank Kimani
  • Joab Ogolla
  • Lucy Gachanja
  • Katherine Damaris
  • Kevin Onyango Omondi
  • Calvin Shikuku Odhiambo
  • Nordeen Abdulghani

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Kenyabuzz Limited. "Movies now showing in Kenya by — KenyaBuzz Movies". KenyaBuzz (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2022-08-09. 
  2. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-03-02. Iliwekwa mnamo 2022-08-09.