Nenda kwa yaliyomo

Nguva

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Sirenia)
Nguva
Nguva wa kawaida
Nguva wa kawaida
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Nusungeli: Theria
Oda ya juu: Afrotheria
Oda: Sirenia
Illiger, 1811
Ngazi za chini

Familia 2, jenasi 3 na spishi 5:

Nguva ni wanyama wakubwa wa oda Sirenia wanaoishi baharini. Hata hivyo ni mamalia wanaozaa watoto walio hai na kuwalisha kwa maziwa. Nguva huwa na mikono ya mbele na mkia wenye umbo la pembetatu. Wanaishi kwenye pwani za Bahari ya Hindi, Bahari ya Karibi, Afrika ya Magharibi na mto wa Amazonas. Wanaweza kufikia urefu wa mita 2.5 hadi 4 na uzito wa kg 1,500.

Wanahatarishwa kutokana na uwindaji hivyo wanalindwa kila nchi.

Jina la Kisayansi Sirenia linatoka na neno la Kigiriki Σειρῆνες Seirēnes. Neno la "nguva" pia ina maana ya mtu mwenye mwili wa mwanamke na mkia wa samaki kama sireni wa mitholojia ya Kigiriki. Hula manyasi ya bahari na mimea ya maji mingine.

Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.