Shikomor
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Shikomor ni lugha asilia ya wakazi wa funguvisiwa ya Komori katika Bahari Hindi. Pamoja na Kifaransa na Kiarabu ni moja ya lugha rasmi ya Komori.
Inahesabiwa kati ya lahaja za Kiswahili au kama lugha ya karibu na Kiswahili. Huandikwa kwa herufi za Kiarabu lakini kuna pia mielekeo ya kusanifisha maandishi yake kwa herufi za Kilatini.
Kwa jumla athira ya Kiarabu na Kifaransa ilikuwa kubwa hivyo kuna maneno mengi zaidi ya asili ya Kiarabu kuliko kwenye Kiswahili sanifu.
Kila kisiwa cha Komori huwa na lahaja yake zinazoitwa:
- Grande Comore - Shingadzija
- Anjouan - Shindzuani
- Mohéli - Shimwali
- Mayotte - Shimaore