Sedekia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sedekia alivyochorwa na Guillaume Rouillé katika Promptuarii Iconum Insigniorum

Sedekia (kwa Kiebrania צִדְקִיָּהוּ, Tsidkiyyahu|Ṣiḏqiyyā́hû, "Haki yangu ni YHWH"; kwa Kigiriki Ζεδεκίας, Zedekías; kwa Kilatini Sedecias), alikuwa mfalme wa mwisho wa Yuda.

Alikuwa mwana wa mfalme Yosia na kuitwa awali Matania.

Kisha kuwekwa madarakani na Nebukadneza II, mfalme wa Babuloni, kwa kiapo cha kuwa mwaminifu kwake, aliasi na kusababisha Yerusalem izingirwe tena na jeshi na hatimaye itekwe na kuteketezwa mwaka 597 KK.

Ilitokea hivyo kwa sababu Sedekia alishindwa kutekeleza maelekezo aliyopewa na nabii Yeremia, ambaye utabiri wake ulitimia daima, lakini mfalme aliogopa mawaziri wake waliomuendesha walivyotaka. Kwa kushindwa kutii Neno la Mungu na kwa kuvunja kiapo chake, Biblia inamhukumu kwamba "alitenda yaliyo mabaya mbele ya Bwana". (2Fal 24:19-20; Yer 52:2-3)

Nebukadneza aliagiza watoto wote wa Sedekia wauawe mbele yake na hatimaye alimpofusha na kumpeleka uhamishoni Mesopotamia alipobaki hadi kufa.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sedekia kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.