Saint Vincent (kisiwa)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nyumba kisiwani St. Vincent

Saint Vincent ni kisiwa cha Antili Ndogo katika bahari ya Karibi kati ya Saint Lucia na Grenada.. Ni kisiwa kikuu cha nchi ya Saint Vincent na Grenadini. Asili yake ni ya kivolkeno.

Mji mkubwa ni Kingstown mwenye wakazi 19,300. Kwa jumla kuna wakazi 110,000.

Mlima mkubwa kisiwani ni volkeno ya La Soufrière iliyolipuka 1812 na 1902 ilipoua watu 1,680. Mlipuko wa mwisho ulitokea 13 Aprili 1979.