Punyeto

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Vifaa vya kujichulia vikiwa dukani [1].

Punyeto ni tendo lolote la kujitafutia ashiki binafsi hasa kwa kuchochea viungo vya uzazi. Wanaochukua hatua hiyo ili wajipatie kionjo cha kuridhisha kinachofanana na kile cha tendo la ndoa kwa kawaida wanasukumwa na msisimko uliowapata, pamoja na haya ya kujitafutia mwenzi na hofu ya kuambukizwa maradhi ya zinaa.

Tathmini mojawapo[hariri | hariri chanzo]

Kufanya hivyo ni kupotosha maana ya jinsia kwa binadamu, ambayo ni kufanya wawili wawe kitu kimoja kwa nguvu ya upendo ambao uanze rohoni na kukamilika katika muungano wa miili yao.

Upendo maana yake ni kujitoa kwa muungano na mpenzi unaoleta tunda lake katika mtoto, ambaye ni kwa pamoja wa baba na wa mama, akiwaunganisha upya ndani mwake.

Katika tendo la kujichua hakuna lolote kati ya hayo: hakuna upendo wala kujitoa kwa wengine, hakuna muungano wala uzazi, isipokuwa kujitafutia iwezekanavyo furaha ya kimwili (ashiki) iliyokusudiwa na Mungu kuwa sehemu ya furaha nzima ya muungano wa ndoa.

Katika tendo hilo la ubinafsi mtu yuko peke yake na kubaki peke yake: halengi chochote nje ya mwili wake, hivyo anazidi kuzama ndani mwake badala ya kustawi kwa kujiwekea malengo mema (k.mf. ndoa, haki, huduma kwa wenye shida, utume n.k.). Matokeo yake ni kupoteza nguvu za mwili na hasa kuvuruga msimamo wa nafsi kwa kujisikia mnyonge, mwenye kosa na mtumwa wa tendo ambalo analikinai mara tu baada ya kulitenda. Hatimaye anaweza kupata matatizo katika tendo la ndoa.

Kwa msingi huo Kanisa Katoliki linahesabu punyeto kuwa dhambi kubwa, tena upande mmoja ni kubwa kuliko uasherati (kuzini kati ya msichana na mvulana), kwa sababu linakwenda kinyume cha maumbile na kuandaa njia kwa dhambi nyingine (k.mf. ushoga)[2].

Hata hivyo elimunafsia inatueleza pia urahisi kwa mtu asiyekomaa kimapendo kufuata njia hiyo danganyifu, tena ngumu kuachwa baada ya kuzoeleka mpaka ukawa uraibu wa punyeto[3].

Ndiyo sababu Kanisa linamhimiza padri kupokea kwa huruma wenye tatizo hilo na kuwasaidia mashauri ya kibinadamu pia kuhusu afya ya mwili na ya nafsi. Kwa mfano: kunyosha viungo kwa kazi za mikono au kwa michezo, kulalia pagumu tena si kifudifudi, kukwepa vinywaji vinavyochochea neva (kahawa, chai n.k.), kushirikiana zaidi na watu, kusaidia wenye shida. Upande wa roho awashauri kufuata vizuri dini. Awatumainishe wanaweza kushinda, kwa hiyo wasikate tamaa wala wasiogope mno.

Kutumia punyeto kunaweza kuleta matatizo kwa njia ya uzazi na kushindwa kueneza mbegu za uzazi wakati wa kujamiana[4]</ref>.

Tathmini tofauti[hariri | hariri chanzo]

Hata hivyo kuna madaktari wanaohimiza punyeto na kusema ni njia ya kuonyesha pendo binafsi na ni kitendo cha kawaida kabisa kisicho na madhara yoyote katika maumbile ya uzazi. Tena wanasema mtu anapopiga punyeto kemikali ya endofini hutolewa ambayo inafanana na dawa za kulevya na hivyo husaidia kwa muda mfupi kupunguza maumivu na msongo wa mawazo.

Watu wengine wanatetea punyeto na kuipendekeza kama njia ya kuzuia uenezi wa ukimwi.

Bila shaka wanaofanya biashara ya vifaa vya kujichulia na ponografia wako mstari wa mbele kuhimiza punyeto tangu utotoni.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Those who insert objects as aids to masturbation risk them becoming stuck (e.g. as rectal foreign bodies). Men and women can fall prey to this problem. A woman went into a German hospital with two pencils in her bladder, having pierced her urethra after inserting them during masturbation. Cfr. Wegner, HE; Franke M; Schick V. (May 1997). "Endoscopic removal of intravesical pencils using percutaneous nephrolithotomy sheath and forceps". Journal of Urology 157 (5): 1842. PMID 9112540. doi:10.1016/s0022-5347(01)64878-x. 
  2. Katekisimu ya Kanisa Katoliki, "Article 6: The Sixth Commandment", cfr. www.vatican.va. p. 2352, inafundisha: "By masturbation is to be understood the deliberate stimulation of the genital organs in order to derive sexual pleasure. "Both the Magisterium of the Church, in the course of a constant tradition, and the moral sense of the faithful have been in no doubt and have firmly maintained that masturbation is an intrinsically and gravely disordered action." "The deliberate use of the sexual faculty, for whatever reason, outside of marriage is essentially contrary to its purpose." For here sexual pleasure is sought outside of "the sexual relationship which is demanded by the moral order and in which the total meaning of mutual self-giving and human procreation in the context of true love is achieved." To form an equitable judgment about the subjects' moral responsibility and to guide pastoral action, one must take into account the affective immaturity, force of acquired habit, conditions of anxiety or other psychological or social factors that lessen, if not even reduce to a minimum, moral culpability."
  3. Ferguson, Sian (27 January 2020). Is 'Masturbation Addiction' Possible?.
  4. According to DSM-5-TR, "Delayed ejaculation is associated with highly frequent masturbation, use of masturbation techniques not easily duplicated by a partner, and marked disparities between sexual fantasies during masturbation and the reality of sex with a partner." Cfr. "American Psychiatric Association 2022 ch. 16": American Psychiatric Association (2022). "Sexual Dysfunctions". Diagnostic and Statistical Manual of Mental Disorders, Fifth Edition, Text Revision (DSM-5-TR(tm)). G - Reference, Information and Interdisciplinary Subjects Series. American Psychiatric Association Publishing. p. 479. ISBN 978-0-89042-576-3.