Nyota ya asubuhi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Nyota ya asubuhi (morning star) ni jina linalotumiwa sana na watu tofauti na kwa maana mbalimbali.

Kwa kawaida linataja sayari ya Zuhura (Venus) ambayo mara nyingi ni nyota ya mwisho inaoonekana angani kabla ya mapambazuko ya Jua kutokana na mwangaza wake mkubwa. Kwa sababu hiyohiyo Zuhura huitwa pia "nyota ya jioni“ ikionekana kabla ya kufika kwa giza jioni.

Katika Kitabu cha Ufunuo imeandikwa kuwa Yesu alijitambulisha kwa jina hilo pia (22:16) na kwamba aliahidi nyota ya asubuhi kwa yule "atakayeshinda na kuendelea kufanya kazi zake (za Yesu) hadi mwisho" (2:28).

Katika Qurani, Sura 86 (at-Tariq) neno الطارق al-tariq linachukuliwa mara nyingi kwa maana ya "nyota ya asubuhi".[1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Linganisha Lane, Arabic-English Lexicon, 1893, digitized onlibe version Perseus Collection Arabic Materials, uk. 1886; " الطارق mentioned in the Kur [lxxxvi. 1 and 2], The star that appears in the night: (Er-Rághib, O:) or the morning-star; (S, O, K;) because it comes [or appears] in [the end of] the night"