Nyanda za juu za Ngorongoro

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya nyanda za juu za Ngorongoro, inatazamwa kutokea kaskazini kuelekea kusini.

Nyanda za juu za Ngorongoro (kwa Kiingereza: Ngorongoro Highlands au Crater Highlands) ni eneo lenye miinuko lililopo kwenye bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki katika mikoa ya Arusha na Manyara, kaskazini mwa Tanzania.

Jiolojia[hariri | hariri chanzo]

Nyanda za juu za Ngorongoro zinapatikana katika mgawanyiko ambapo bamba la Afrika linagusana na bamba la Somalia, kukutana kwa mabamba haya mawili husababisha maumbile mapya ya kijiolojia kujitokeza.[1]

Kama ilivyo kawaida, sehemu za mgawanyiko kati ya mabamba ya gandunia, maumbile ya kivolkeno huwepo. Hivyo nyanda hizo zina kasoko nyingi na kaldera za kivolkeno. Magma, hupanda kupitia nyufa zilizotokea na kufika kwenye uso wa ardhi na kuunda umbo la koni. Kaldera huundwa pindi volkeno ikilipuka au kuporomoka ndani yake.[1]

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Yafuatayo hupatikana kwenye nyanda za juu za Ngorongoro:

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 "Crater Highlands". NASA Earth Observatory. Iliwekwa mnamo 29 September 2017.  Check date values in: |accessdate= (help)