Algae

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mwani)
Rukia: urambazaji, tafuta
Dinobryon ni algae wa jamii ya Chrysophyceae
Mwani ya Laurencia katika hadubini: matawi yaki ni mfuatano wa seli za pekee na yote ina unene wa 1 mm pekee.
Algae aina ya phytoplankton zikiota kama maua katika Atlantiki ya Kusini mbele ya Argentina

Algae (umoja ni alga, uwingi algae; pia: mwani) ni jina la kundi kubwa la viumbehai vidogo kati ya protista sana vinavyofanana na mimea. Zina uwezo wa kujilisha kwa njia ya usanisinuru yaani hutengeneza chakula chao kwa msaada wa mwanga wa jua.

Kuna aina nyingi sana za algae nyingine zina seli moja tu na nyingine zina seli nyingi. Aina kubwa zinajulikana kama mwani za baharini. Katika uwezo wa usaninisinuru zinalingana na mimea lakini hukosa viungo vingi vilivyo kawaida kati ya mimea hivyo katika taksonomia au mpangilio wa spishi hazihesabiwi kati ya mimea.

Algae hazina majani, mizizi na viungo vyingine vya mimea.

Marejeo [hariri]