Mauaji ya Halaiki ya My Lai
Mauaji ya Halaiki ya My Lai (kwa Kiingereza: The My Lai Massacre; tamka: [mi.˧˩˥'lɐːj˧˧], Thảm sát Mỹ Lai, Thảm sát Sơn Mỹ) yalikuwa mauaji ya mamia ya watu yaliyofanywa na kikosi cha majeshi ya Marekani katika kijiji cha My Lai, nchini Vietnam Kusini tarehe 16 Machi 1968. Katika kumbukumbu za My Lai yameorodheshwa majina ya wahanga wapatao 504.
Mauaji ya My Lai
[hariri | hariri chanzo]Siku ile kikosi cha wanajeshi wa Marekani chini ya uongozi wa Luteni William Calley walipewa amri ya kutafuta wanamgambo wa Vietkong kijijini wakiambiwa ya kwamba Vietkong walijificha katika eneo lile. Waliambiwa ya kwamba wasingekuta watu raia mle lakini wategemee wanamgambo. Kikosi kilipoingia My Lai hawakuona wanamgambo bali wanawake, watoto na wazee watupu. Wakihofia ya kwamba Vietkong wanajificha kwenye vibanda na nyumba wanajeshi kadhaa walianza kufyatulia risasi kwenye nyumba na mauaji wa kwanza ya wanawake na watoto yalitokea kwa njia hiyo. Baada ya kusikia risasi watu walianza kukimbia kila upande na wanajeshi wengine walipiga risasi kwa wakimbiaji. Baada ya muda kidogo sehemu ya askari waliendelea kuwaua watu wote. Wakapitia nyumba kwa nyumba na kuua wajeruhiwa pia.
Wavietnam 11 waliokolewa na rubani wa helikopta ya Kimarekani aliyeona mauaji kutoka hewani. Alishuka akajaza helikopta na Wavietnam wachache waliobaki akitisha askari wenzake kuwapigia bunduki wakijaribu kuwaua. Rubani aliyeitwa Hugh Thompson alitoa taarifa kwa wakubwa wake.
Kufichwa kwa tendo
[hariri | hariri chanzo]Taarifa hii pamoja na habari zote zilizohusu mauaji haya zilifichwa ndani ya jeshi. Jenerali mhusika aliagiza taarifa rasmi lakini afisa aliyefanya utafiti aliandika ya kwamba kikosi cha Luteni Calley ilikuwa na mapigano makali huko My Lai kikaua maadui Vietkong 128 na watu raia 22 waliuawa kwa bahati mbaya.
Kesi ilifunguliwa
[hariri | hariri chanzo]Habari za My Lai zilifichuliwa kwa sababu askari mwingine aliyeungwa baadaye na kikosi cha Calley ingawa hakuwepo My Lai alisikia hadithi nyingi kutoka wenzake na baada ya kuondoka jeshini aliandika barua kwa ofisi ya raisi ya Marekani na wabunge mbalimbali wa Washington alipoeleza habari za My Lai. Mbunge mmoja tu alifuatilia barua akasababisha utafiti rasmi na Luteni Calley pamoja na askari 25 wengine walifunguliwa kesi za jinai ya uuaji.
Tangu Desemba 1969 magazeti ya Marekani yalianza kutuoa taarifa juu ya mauaji ya My Lai. Watu wengi huko nchini na pia duniani kwa jumla walishtuka sana.
Kesi 4 zilifunguliwa mbele ya mahakama ya kijeshi na 1971 Luteni Calley pekee yake alihukumiwa akapewa jela kwa maisha. Lakini rais Nixon aliamua ya kwamba atakaa muda wa jela kwake nyumbani chini ya ulinzi na mwaka 1974 Calley alisamehewa adhabu na rais.
Matokeo ya baadaye
[hariri | hariri chanzo]Taarifa za My Lai ziliongeza mkasi upinzani dhidi ya vita ya Vietnam ndani ya Marekani.
Leo hii kuna makumbusho mahali pa kijiji cha kale kilichojengwa na shirika la wanajeshi wa zamani wa Marekani.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- An American Tragedy Archived 30 Machi 2008 at the Wayback Machine.
- The My Lai Courts-Martial 1970 Archived 16 Aprili 2003 at the Wayback Machine.
- Into the Dark: The My Lai Massacre Archived 11 Mei 2008 at the Wayback Machine.
- 1969 TIME article Archived 13 Oktoba 2007 at the Wayback Machine.
- 'Blood and fire' of My Lai remembered 30 years later
- My Lai Peace Park Project Archived 9 Mei 2008 at the Wayback Machine.
- The first public reports by journalist Seymour Hersh about the My Lai Massacre for the St. Louis Post Dispatch, 13 November, 20 Novemba and 25 Novemba 1969. Archived 15 Julai 2011 at the Wayback Machine.
- ↑ Report of the Department of Army review of the preliminary investigations into the Mỹ Lai incident. Volume III, Exhibits, Book 6—Photographs, 14 March 1970. From the Library of Congress, Military Legal Resources.
- ↑ "My Lai", Original broadcast PBS American Experience, 9 pm, April 26, 2010 Time Index 00:35' into the first hour (no commercials)
- ↑ "Report of the Department of the Army Review of the Preliminary Investigations into the My Lai Incident