Majadiliano ya mtumiaji:Suzane l mollel

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

Idd ninga (majadiliano) 00:35, 9 Juni 2021 (UTC)[jibu]

Kupitia Makala[hariri chanzo]

Salamu, Hongera sana kwa juhudi katika kuanzisha makala katika Wikipedia ya Kiswahili, kwa sasa ni vyema sana ukapitia mara kwa mara makala ambazo umezianzisha ili kuona mabadiliko yaliyofanyika na kisha uyatumie katika makala zako nyingine, pia, kama unataka kuweka jamii unatakiwa kutumia hizi alama ([[]]) badala ya kuweka ({{}}), Amani Sana Idd ninga (majadiliano)

Usitafsiri neno kwa neno[hariri chanzo]

Dada umetafsiri sehemu za Uwanja wa michezo wa Agege neno-kwa-neno na hivyo kuandika sentensi mbaya ambazo si Kiswahili kweli. Usitafsiri kamwe neno kwa neno. Kama Kiingereza chako hakitoshi, acha! Tafakari sentensi inamaanisha nini, halafu sema kwa maneno yako. Usipoelewa usitafsiri. Usifuate muundo wa lugha ya kigeni ukitunga Kiswahili!!

Halafu utambue ukiona makala ya Kiingereza yenye makosa. Hiyo ya Agege inasema "State Government of Lagos says that efforts are being made to complete their up-gradation of the stadium in February". Je hutambui kosa? Haisemi tangazo hili ni ya mwaka gani. Ni bure na kosa kutaja mambo haya katika makala ya Kiswahili, maana tangazo ni ya mwaka 2015 (!!!) na wewe unaandika sasa kama ni tangazo la mambo yanayokuja. Unaweza kuona tarehe ya tanbihi, utaona 2015. Kwa nini unatafsiri habari ya aina hii isiyo na maana yoyote??? Kipala (majadiliano)

Picha ya Maria Stewart[hariri chanzo]

Salamu, katika makala hii https://sw.wikipedia.org/wiki/Maria_W._Stewart umeweka picha ambayo inaonekana haina mahusiano na makala, jaribu kuipitia makala hiyo na picha ili kuondoa mashaka na kama picha hiyo haina mahusiano ni heri kuiondoa mara moja, ,pia angalia picha katika makala hii hapa https://sw.wikipedia.org/wiki/Louise_Miller, je unadhani inamahusiano na makala, pitia pia na makala hii hapa https://sw.wikipedia.org/wiki/Janet_Cooke, ni vyema kuzifanyia maboreshe makala hizi kuliko kuendelea kuweka picha zenye mashaka ?Idd ninga (majadiliano)

Marekebisho[hariri chanzo]

Hello, hebu pitia kwanza makala zako unazoweka picha na kuzirekebisha, hakikisha unaweka picha za kweli ili kuondoa usumbufu,picha unazowka nyingine hazina mahusiano kabisa na makala,ni heri kufanya hivyo kuliko kuendeleza makala na kuziharibu Idd ninga (majadiliano)

Kuhusu Hashtag[hariri chanzo]

Angalia makala hii hapa https://sw.wikipedia.org/wiki/Tamron_Hall , kama utapitia makala kwa ajili ya shindano la picha na ukawa umefanyia marekebisho picha ambayo tayari kapaki mtu mwingine, siyo vyema kuweka hashtag, ni bora uweke hashtag katika makala ambayo umepakia picha wewe mwenyewe,lakini pia katika makala hii hapa https://sw.wikipedia.org/wiki/Taylor_Terrell umeweka picha ya Tylor Marsh ambae ni watu wawili tofauti na mtu anaeelezewa katika makala, sasa kama utaona kuwa kuna changamoto ya kupata makala iliyopo katika Wikipedia ya Kiingereza, basi acha makala hiyo bila kuiweka picha, Amani sana, Idd ninga (majadiliano)