Lango:Hip hop/Wasifu uliochaguliwa/Kool G Rap

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Cool G. Rap akiwa na rapa the Game
Cool G. Rap akiwa na rapa the Game

Nathaniel Thomas Wilson (amezaliwa tar. 20 Julai, 1968), anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Kool G Rap (au kwa kifupi huitwa G Rap), Kool G. Rap, na Giancana (Maana ya kifupisho cha "'G."'), ni rappa, kutoka mjini Corona jirani na mji wa Queens, New York huko nchini Marekani. Ameanza shughuli zake za kurap katikati mwa miaka ya 1980 akiwa kama nusu ya kundi la Kool G Rap na DJ Polo na pia akiwa kama mwanachama wa Juice Crew.

Mara kwa mara huhesabiwa kama miongoni mwa Ma-MC wenye athira na maarifa ya juu wa muda wote, akiwa kama mwanzilishi wa staili ya mafioso rap/street/hardcore na uimbaji wa silabinyinginyingi. Kwenye albamu yake ya The Giancana Story, ameeleza ya kwamba herufi "G" katika jina lake humaanisha "Giancana" (kajipa jina la jambazi sugu Sam Giancana), lakini kwa namna nyingine mwenyewe eti anadai lina-maanisha "Genius".

Pia amewahi kutajwa na wasanii maarufu wa hip hop kama vile Eminem, Nas, Jay Z, Big Pun, RZA na wengine wengi tu.

Soma zaidi....