Ladino

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ladino (pia: Kihispania ya Kiyahudi) ni lugha inayozungumzwa na Wayahudi katika nchi mbalimbali. Ni lugha ya karibu na [Kihispania] ikiwa na maneno ya Kiebrania ndani yake. Wasemaji wengi wako Israel, halafu Uturuki, Bulgaria na Marekani. Idadi ya wasemaji inaendelea kupungua; mnamo 1990 walikuwa 150,000 duniani.

Asili ya lugha hii ni jumuiya kubwa ya Wayahudi walioishi Hispania hadi karne ya 15. Hadi mwaka 1492 sehemu za Hispania ilitawaliwa na Waarabu. Baada ya kutekwa kwa nchi yote na Wahispania Wakristo walianza kuwa na wasiwasi kuhusu Waarabu Waislamu na pia Wayhudi waliokaa nchini. Matso makali yalifuata na dini zote nje ya Ukristo wa kikatoliki zilipigwa marufuku. Waislamu na Wayahudi wengine walikuwa Wakristo lakini wengi waliondoka Hispania na kukimbilia nchi za nje.

Kwa njia hii Wayahudi wenye lugha ya Kihispania walifika katika nchi za Ulaya ya Magharibi na Milki ya Osmani kuanzia Afrika ya Kaskazini hadi Uturuki. Walijenga sinagogi zao wakaendelea kutumia Kihispania chao.

Zamani lugha iliandikwa kwa herufi za Kiebrania lakini nje ya Israeli huandikwa kwa alfabeti ya Kilatini.

Ladino imetunza maneno mengi ya Kihispania cha Kale.

Jumuiya za Wayahudi waliotumia Kiladino ziliathiriwa vibaya sana na maangamizi makuu dhidi ya Wayahudi wa Ulaya mnamo 1941-1945 wengi waliuawa.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]