Kipululu
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
-Kwa kiunzi cha binadamu tazama makala "Kiunzi cha mifupa"-
| Kipululu | ||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
|
Vipululu ni ndege wa familia Turnicidae. Spishi moja inaitwa kiunzi pia (tazama orodha ya spishi). Ndege hawa wanafanana tombo lakini hawana mnasaba na hawa. Wana rangi ya mchanga na madoa meusi au kahawia. Hawapendi kupuruka. Jike ana rangi kali kuliko dume na huanzisha ubembelezi. Dume huatamia na hutunza makinda.
Ndege hawa waliainishwa zamani ndani ya Gruiformes (oda ya makorongo) au Galliformes (oda ya kuku). Lakini utafiti wa ADN umeonyesha kama vipululu wana mnasaba na vitwitwi. Kwa hivyo wanaainishwa ndani ya Charadriiformes sasa. Kisukuku kimefunuliwa ambacho kimetambuliwa kama jamaa wa vipululu na kuitwa Turnipax.
[hariri] Spishi za Afrika
- Ortyxelos meiffrenii, Kiunzi (Lark Buttonquail or Quail Plover)
- Turnix hottentottus, Kipululu Kiuno-cheusi (Hottentot or Black-rumped Buttonquail)
- Turnix nigricollis, Kipululu wa Malagasi (Madagascar Buttonquail)
- Turnix sylvaticus, Kipululu Macho-njano (Small or Kurrichane Buttonquail or Andalusian Hemipode)
[hariri] Spishi za mabara mengine
- Turnix castanota (Chestnut-backed Buttonquail)
- Turnix everetti (Sumba Buttonquail)
- Turnix maculosa (Red-backed Buttonquail)
- Turnix melanogaster (Black-breasted Buttonquail)
- Turnix ocellata (Spotted Buttonquail)
- Turnix olivei (Buff-breasted Buttonquail)
- Turnix pyrrhothorax (Red-chested Buttonquail)
- Turnix suscitator (Barred Buttonquail)
- Turnix tanki (Yellow-legged Buttonquail)
- Turnix varia (Painted Buttonquail)
- Turnix velox (Little Buttonquail)
- Turnix worcesteri (Philippine Buttonquail)