Kelvin Yondan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kelvin Yondan (amezaliwa 4 Oktoba 1984), ni mchezaji wa mpira wa miguu kutoka nchini Tanzania. Anacheza nafasi ya beki wa kati. Pia anamudu nafasi ya kiungo.

Amechezea klabu ya Yanga Sc na Polisi Tanzania nchini Tanzania. Pia anachezea timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars.

Yondani ni mmoja kati ya wakongwe wakudumu ndani ya ligi kuu ya soka Tanzania bara kwa miaka mingi akiwa katika ubora.

Timu alizowahi kuchezea

Aina ya uchezaji

Ni mmoja kati ya mabeki bora Afrika Mashariki, kwa zaidi ya miaka kumi sasa anaunda ukuta imara wa Wanajangwani Yanga. Anakaba kwa nguvu mipira ya juu na chini na undava wa hali ya juu. Anafahamika kwa tackling kali na kuanzisha mashambulizi tokea nyuma.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kelvin Yondan kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.