Nenda kwa yaliyomo

Kanisa kuu la Mtakatifu Yosefu, Dar es Salaam

Majiranukta: 6°49′10″S 39°17′17″E / 6.81944°S 39.28806°E / -6.81944; 39.28806
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kanisa la Mtakatifu Joseph)
Kanisa kuu la Mt. Yosefu.
Kanisa kuu kati ya maghorofa ya kisasa ya Dar es Salaam.

Kanisa kuu la Mtakatifu Joseph (kwa Kiingereza: St Joseph Cathedral church) ni kanisa lililopo katika Mkoa wa Dar es Salaam, Wilaya ya Ilala, mkabala na Sokoine Drive, likiangalia Waterfront, karibu na geti la boti zinazoelekea Zanzibar.

Kanisa hili lilijengwa kwa umahiri na wamisionari Wabenedikto kuanzia mwaka 1897 hadi 1902[1] likatabarukiwa mwaka 1905.[2]. Hadi sasa ni kanisa kuu la Jimbo Kuu la Dar es Salaam.

Mtindo uliofuatwa ni mtindo wa Kigothi mamboleo. Kati ya sifa zake, mojawapo ni vioo vya rangi nyuma ya altare[3].

  1. Michael Hodd, East Africa Handbook: The Travel Guide, p. 344
  2. (Kiitalia) St. Benedict Monastery Archived 2012-08-02 at Archive.today
  3. St. Joseph's Cathedral at Lonely Planet

6°49′10″S 39°17′17″E / 6.81944°S 39.28806°E / -6.81944; 39.28806

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu: