Jaka Mwambi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jaka Mwambi

Nchi Tanzania
Kazi yake Mwanasiasa na Mwanadiplomasia


Jaka Mgwabi Mwambi (1950-2019) alikuwa mwanasiasa na mwanadiplomasia wa nchini Tanzania, aliyepata kuwa mkuu wa mkoa wa Rukwa, Tanga na Iringa na makamu katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi.[1] hadi pale nafasi yake ilipochukuliwa na aliyekuwa mbunge wa Newala, mnamo mwezi Novemba 2007.

Mwambi aliteuliwa kuwa balozi wa Tanzania nchini Urusi tarehe 21 Julai 2008[2] akawasilisha hati za utambulisho wa ubalozi kwa rais wa Urusi Dmitry Medvedev tarehe 18 Septemba 2008.[3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]