Isoken Ogiemwonyi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Isoken Ogiemwonyi ni mwanamitindo wa Nigeria, mwanzilishi na mratibu wa lebo ya kimitindo iitwayo "Obsidian", na duka liitwalo "ZAZAII". Pia anajulika kama muanzilishi msaidizi wa Winterfell Ltd,ambayo huratibu na kuhodhi Le Petit Marche ya nchini Naijeria na L’Espace trademarks. Ni mshindi wa 2012 MTN Lagos Fashion & Design Week na British Council Young Creative Entrepreneur of the Year. Mnamo mwaka 2013, The Guardian ilimueka nafasi ya 25 ya wanawake wenye ushawishi mkubwa barani Afrika.[1]

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Alimaliza elimu yake na kutunukiwa shahada ya sheria katika Chuo kikuu cha Nottingham.Pia ana diploma ya uzamili katika usimamizi wa ukarimu katika Glion Institute of Higher Education, Switzerland. Pia ana astashahada kutoka chuo cha Malvern.

Maisha ya Kazi[hariri | hariri chanzo]

Isoken ni mhariri BellaNaija mitindo na anafanya kazi ya uhariri wa mambo ya kibiashara katika BNStyle.[2] Isoken na Wonuola Odunsi ni waanzilishi wasaidizi wa Winterfell Ltd, ambayo inahodhi Le Petit Marche ya nchini Naijeria na L’Espace trademarks.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Ifeachor, Adaobi; Allen, Paddy (2013-03-08). "Africa's top women achievers - nominated by you". the Guardian (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-11-18. 
  2. "Isoken Ogiemwonyi". BN Style (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2020-11-19. 
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Isoken Ogiemwonyi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.