Ilolangulu (Mbogwe)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Ilolangulu (Bukombe))

Kwa maana nyingine ya jina hili angalia hapa

Ilolangulu ni mojawapo kati ya kata zinazounda halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe katika Mkoa wa Geita, Tanzania. Msimbo wa posta ni 30414.

Kata hii inaundwa na vijiji 4 na wakazi wa eneo hili ni hasa wa makabila ya Wasumbwa, Wasukuma na Waha na ndiyo kata aliyozaliwa mbunge wa jimbo la Mbogwe, Augustine Manyanda Masele.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 16,584 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 11,703 waishio humo. [2]

Wakazi wa kata hii ni wakarimu na wanajihusisha na shughuli za kilimo na ufugaji. Wanalima nyanya, pamba, tikiti na mahindi.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Kata za Wilaya ya Mbogwe - Mkoa wa Geita - Tanzania

Bukandwe | Bunigonzi | Ikobe | Ikunguigazi | Ilolangulu | Iponya | Isebya | Lugunga | Lulembela | Masumbwe | Mbogwe | Nanda | Ngemo | Nhomolwa | Nyakafulu | Nyasato | Ushirika

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Geita bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.