Historia ya Gibraltar

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Historia ya Gibraltar ni kwamba rasi hiyo muhimu ilikuwa sehemu ya Hispania kati ya miaka 1501 na 1704.

Mwaka 1704 wakati wa vita kati ya Hispania na Uingereza ilitwaliwa na Waingereza na Waholanzi.

Mwaka 1713 Hispania ilikubali katika amani ya Utrecht kuwa rasi itakuwa chini ya mamlaka ya Uingereza.

Hispania imedai mara nyingi kurudishiwa eneo hilo ikishtaki Uingereza kuwa na koloni la mwisho katika Ulaya nzima. Lakini wakazi wenyewe walipigia kura mwaka 2002 hoja ya kubaki upande wa Uingereza badala ya kujiunga na Hispania na zaidi ya 98% wakakubali.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Gibraltar kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.