Hammurabi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Sehemu ya juu ya nguzo ya Hammurabi yenye sheria zake yamwonyesha mfalme Hammurabi mbele ya mungu Marduk.
Babeli, 1792 - 1750 KK

Hammurabi (takr. 1810 KK - 1750 KK) alikuwa mfalme wa sita wa mji wa Babeli akapanusha eneo lake na kuunda milki ya kwanza ya Babeli. Ajulikana hasa kwa mkusanyo wa sheria za Hammurabi ambazo ni kati ya sheria za kwanza za dunia zilizoandikwa.

Hammurabi alirithi ufalme kutoka kwa babaye akitawala eneo la mji wa Babeli kama dola-mji tu. Katika miaka ya utawala wake alifaulu kupanusha himaya yake hadi kutawala Mesopotamia yote. Hivyo alianzisha milki ya kwanza ya Babeli.

Sheria za Hammurabi [hariri]

Umaarufu wake watokana na sheria zake. Hakuwa mtawala wa kwanza wa Mesopotamia alitunza sheria za milki kimaandishi. Lakini sheria nyingine zimepotea au kuhifadhiwa kisehemu tu. Mkusanyiko wa sheria za Hammurabi ni wa kwanza uliosambazwa kiasi cha kuwa na nakala nyingi na nakala kadhaa zimehifadhiwa hadi leo na kutupa picha ya jamii ile ya kale sana.

Nakala maarufu ni nguzo ya jiwe kubwa lenye kimo cha mita 2.25 inayomwonyesha mfalme mbele ya mungu Marduk na chini yake ziko sheria katika mwandiko wa kikabari.

Sheria hizi zilikuwa kali sana. Mfano wake ni vipengele vifuatavyo:

  • na. 3: Anayesimama mahakamani na kutoa ushuhuda katika kesi yenye ashabu ya mauti lakini hawezi kuthebitisha maneno yake atakufa
  • na. 195: Mwana anayempiga baba yake atakatwa mkono
  • na. 196: Anayeharibu jicho la mtu huru atakatwa jicho lake.


Viungo vya Nje [hariri]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Administradors.gif Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hammurabi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.