Fungo-miti wa Afrika
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Fungo-miti | ||||||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Fungo-miti (Nandinia binotata)
|
||||||||||||||||
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
||||||||||||||||
Usambazaji wa fungo-miti
|
Fungo-miti (wa Afrika) (Nandinia binotata) ni mnyama mbua mdogo, spishi pekee ya jenasi yake na ya familia yake Nandiniidae[1]. Ana mwili ufananao na ule wa paka mdogo wenye miguu mifupi, masikio madogo na mkia wa urefu wa mwili. Wanyama wazima huwa na uzito wa kg 1.7 hadi 2.1. Hii ni spishi ya misitu mizito ya Afrika ambapo huishi mitini. Hula vitu vyingi kama wagugunaji, wadudu, mayai, mizoga, matunda, ndege na popo-matunda. Mnyama huyu ni mpweke na hukiakia usiku.
Ijapo fungo-miti anafanana na spishi za fungo za familia Viverridae, inaonekanana kama huyu ni tofauti kwa kinasaba na aliachana na fungo kabla ya paka. Kwa hivyo amepewa jenasi na familia yake binafsi, lakini kuna wataalamu ambao hawakubali.
References [hariri]
- ↑ Wozencraft, W. Christopher (2005). "Order Carnivora (pp. 532-628)". In Wilson, Don E., and Reeder, DeeAnn M., eds. Mammal Species of the World: A Taxonomic and Geographic Reference (3rd ed.). Baltimore: Johns Hopkins University Press, 2 vols. (2142 pp.). ISBN 978-0-8018-8221-0.
| Wikispecies has information related to: Nandinia binotata |
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
| Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Fungo-miti wa Afrika kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |