Eylem Tuncaelli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Eylem Tuncaelli ni mwanaharakati wa kisiasa kutoka Uturuki na mwenyekiti mwenza na msemaji wa chama cha Green Left Party.[1] Alikuwa pia Mwenyekiti wa zamani wa Tawi la Istanbul la Chama cha Uhandisi wa Mazingira.[2]

Biografia[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa mnamo 1975 huko Istanbul. Alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Trakya katika fani ya Uhandisi wa Mazingira mwaka 1999 na mwaka wa 2000 alijiunga na TMMOB (Muungano wa Vyama vya Wahandisi na Wasanifu wa Kituruki). Kati ya 2004 na 2010, alijiunga kama rais wa Tawi la Istanbul la Chama cha Uhandisi wa Mazingira, na kuwa mwanachama hai. Mnamo 2012, pamoja na wengine kama Naci Sonmez, alianzisha chama cha Green Left Party.[2]

Jela[hariri | hariri chanzo]

Mnamo 9 Februari, 2018, yeye na wanachama wengine 10 walikamatwa saa 12 asubuhi, [3][4] wakishutumiwa kwa "kuzalisha uadui kati ya watu" na "propaganda kwa shirika la kigaidi". Wafungwa hao walikuwa wakipinga hatua ya jeshi la Uturuki nchini Syria. Katika mwaka huo huo, waliachiliwa, lakini hati zao za kusafiria zilichukuliwa, na kuwazuia kusafiri Kwenda nchi zingine.[2][5]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Turkish Green co-chairs Eylem Tuncaelli and Naci Sönmez are released". European Greens. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-06-24. Iliwekwa mnamo 2022-02-25.  More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  2. 2.0 2.1 2.2 "Stop the leaders of the Turkish Green Party from being jailed under false charges". European Greens. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-05-23. Iliwekwa mnamo 2022-02-25.  More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  3. "Immediate release of Turkish Green/Left Co-Chairs Eylem Tuncaelli and Naci Sonmez! - Ska Keller, MdEP". skakeller.de. 9 February 2018. Iliwekwa mnamo 2022-02-25.  Check date values in: |date= (help)
  4. "[Green Gazette weekly Turkey digest:] Arrests, Nukes, and banned children's play - Yeşil Gazete". yesilgazete.org. 13 February 2018. Iliwekwa mnamo 2022-02-25.  Check date values in: |date= (help)
  5. "Yeşil Sol Parti Eş Sözcülerinin Pasaportlarına El Konuldu". bianet. Iliwekwa mnamo 2022-02-25. 
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Eylem Tuncaelli kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.