Emirati
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Emirati (Kar.إمارة) ni nchi inayotawaliwa na emir au amiri amabaye ni mtawala kama mtemi anayerithi cheo chake kama mfalme lakini cheo chake hutazamiwa si sawa na mfalme. Jina hili lenye asili ya Kiarabu ni kawaida katika utamaduni wa Kiislamu.
Wakati mwingine inataja pia sehemu ya nchi tu kama inaongozwa na mtu wa familia ya kifalme wa nchi mwenye cheo cha amiri kama mikoa ya Saudia.
Falme za Kiarabu zinajiita "emirati" kwa lugha ya Kiarabu.
Katika historia watawala wa emirati kadhaa walibadilicha cheo chao kuwa mfalme au sultani.
Emirati za kujitawala [hariri]
Emirati za kihistoria [hariri]
- Emirati ya Tiflis
- Emirati ya Sicilia, Sicilia 965-1072
- Emirati ya Granada, Hispania 1228-1492
- Emirati ya Trarza, Mauritania 1640-1910
- Emirati ya Afghanistan, Afghanistan 1996 - 2001
- Az Zubayr
- Bahrain, iliyokuwa ufalme tangu 2002