Ebenezer Andrews

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ebenezer Andrews
Maelezo binafsi
Tarehe ya kuzaliwa 21 Mei 2000
Mahala pa kuzaliwa    Ghana

* Magoli alioshinda

Ebenezer Andrews, (alizaliwa 21 Mei 2000) ni mchezaji wa badminton nchini Ghana.[1] Mnamo Aprili 2019, alikuwa sehemu ya timu ya Ghana ambayo ilishinda taji la shaba katika mashindano ya All Africa Mixed Team Championship ambayo yalifanyika huko Port Harcourt, Nigeria.[2]

Maisha ya awali na elimu[hariri | hariri chanzo]

Andrews alizaliwa 21 mei 2000 huko Winneba, Ghana.[3][4] Ni mwanafunzi wa Chuo kikuu cha ualimu, Winneba.

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Andrews alishiriki katika Mashindano ya Badminton ya Vijana wa Afrika mwaka 2013 (U-19) yaliyofanyika nchini Algeria.[5]

Pia alishiriki katika michezo ya 10 ya All Africa Games katika Chuo Kikuu cha Kenyatta huko Nairobi, Kenya.[6]

Mafanikio[hariri | hariri chanzo]

Andrews na mwenzake Eyram Migbodzi waliwashinda wapinzani wao wa Ivory Coast Doulo Lou Annick na Ousmane Ovedroogo kwa alama 21 –12, 21 –13 na kushinda katika kitengo cha timu mbili za wanaume.[2]

Katika Michezo ya Commonwealth Games mwaka 2018 iliyofanyika nchini Australia, Andrews na mwenzake Daniel Doe walishinda taji la dhahabu katika seti tatu za 2-1 dhidi ya Emmanuel Botwe na Abraham Ayittey katika fainali mara mbili.[7]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Ebenezer Andrews live scores, results, fixtures | Flashscore.com / Badminton". www.flashscore.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-03-01. 
  2. 2.0 2.1 llc, Online media Ghana. "Ghana wins bronze at 2019 All Africa Badminton Mixed Team Champs :: Ghana Olympic Committee". ghanaolympic.org (kwa en-US). Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-03-01. Iliwekwa mnamo 2023-03-01.  More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  3. Afful, Henrietta (2022-03-15). "Ghana Badminton cracks whip: Expels 6, suspends 4". GBC Ghana Online - The Nation's Broadcaster | Breaking News from Ghana, Business, Sports, Entertainment, Fashion and Video News (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2023-03-01. 
  4. GNA. "BAG prepares for Africa Games Qualifiers | News Ghana". https://newsghana.com.gh (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2023-03-01. 
  5. "Ghana to compete in Africa Badminton Junior Championships - MyJoyOnline.com". www.myjoyonline.com (kwa en-US). 2013-03-15. Iliwekwa mnamo 2023-03-01. 
  6. Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named :1
  7. "Ghana Badminton team sweeps victory at Under 19 Championship". The Ghana Guardian News (kwa Kiingereza). Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-03-01. Iliwekwa mnamo 2023-03-01.  More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ebenezer Andrews kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.