Dominic Monaghan
Dominic Monaghan | |
---|---|
Amezaliwa | Dominic Bernard Patrick Monaghan |
Kazi yake | Mwigizaji |
Dominic Bernard Patrick Monaghan (amezaliwa 8 Desemba 1976) ni mwigizaji filamu wa Uingereza. Amepata umaarufu kote duniani kwa kuigiza kama Meriadoc Brandybuck katika filamu ya The Lord of The Rings na pia kama Charlie Pace kwenye kipindi cha Lost. Hivi sasa, anaigiza kama Dr. Simon Campos kwenye kipindi cha FlashForward.
Maisha yake
[hariri | hariri chanzo]Monaghan alizaliwa mjini Berlin, Ujerumani. Wazazi wake ni Maureen na Austin Monaghan, ambaye ni mwalimu wa sayansi.[1] Familia ya Monaghan waliishi katika miji ya Berlin, Dusseldorf-Lohausen, Stuttgart na Münster, wakihamahama kila takriban baada ya kila miaka minne. Baadaye, walihamia katika mji wa Manchester. Monaghan anaongea Kiingereza na Kijerumani vizuri.
Maisha binafsi
[hariri | hariri chanzo]Monaghan anapenda kupanda miti. Yeye anamiliki msitu mdogo nchini India na amefanya kazi kwenye tume za haki za wanyama kama PETA.[2] Monaghan anapenda wadudu, na amefuga wanyama kama kinyonga.[3]
Yeye anapenda kucheza kandanda na mpira wa kikapu. Yeye ni shabiki mkubwa wa timu ya Manchester United. Yeye anaishi mjini Los Angeles, California.
Yeye amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Evangeline Lilly ambaye ni mwigizaji mwenzake wa kipindi cha Lost kuanzia mwaka wa 2004. Mnamo Juni 2008, Monaghan alisafiri pamoja na Lilly mpaka nchi ya Argentina ili kurekodi filamu ya Caiga Quien Caiga.[4] Mnamo Juni 2009, yeye na Evangeline walisafiri pamoja kwenda Rwanda. Vilevile, wawili hawa wanaonekana pamoja mjini Vancouver.
Filamu
[hariri | hariri chanzo]Mwaka | Filamu | Aliigiza kama | Maelezo |
---|---|---|---|
1997 | Hostile Waters | Sasha | |
2001 | The Lord of the Rings: The Fellowship of the Ring | Meriadoc Brandybuck | |
2002 | The Lord of the Rings: The Two Towers | Meriadoc Brandybuck | |
2003 | The Lord of the Rings: The Return of the King | Meriadoc Brandybuck | Alishinda tuzo la Screen Actors Guild Award |
An Insomniac's Nightmare | Jack | ||
2004 | Spivs | Goat | |
The Purifiers | Sol | ||
2005 | Ringers: Lord of the Fans | Mtangazaji | |
Shooting Livien | Owen Scott | ||
2008 | I Sell The Dead | Arthur Blake | |
2009 | X-Men Origins: Wolverine | Chris Bradley / Bolt | |
2011 | Pet | Seth |
Vipindi
[hariri | hariri chanzo]Mwaka | Kipindi | Aliigiza kama | Maelezo |
---|---|---|---|
1996 - 1998 | Hetty Wainthropp Investigates | Geoffrey Shawcross | |
2000 | This is Personal: The Hunt for the Yorkshire Ripper | Jimmy Furey | |
Monsignor Renard | Etienne Pierre Rollinger | ||
2004 - 2010 | Lost | Charlie Pace | Mhusika mkuu tangu 2004 - 2007. Alishinda tuzo la Screen Actors Guild Award. |
2008 | MADtv | Mwenyewe | Mnamo 26 Aprili 2008 |
2008 | Caiga Quien Caiga | Mwenyewe | 23 Juni 2008. Pamoja na Evangeline Lilly |
2009 | Chuck | Tyler Martin | Kipindi kimoja |
FlashForward | Dkt. Simon Campos |
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Lost Boy". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-12-25. Iliwekwa mnamo 2010-01-28.
{{cite web}}
: Unknown parameter|=
ignored (help) Archived 25 Desemba 2008 at the Wayback Machine. - ↑ "Lost Star Dominic Monaghan Appears in New PETA Wildlife Ad". HelpingAnimals.com. Iliwekwa mnamo 21 Februari 2008.
- ↑ http://www.contactmusic.com/news.nsf/article/monaghan%20chameleon%20pets%20tearful%20goodbye_1032678
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-03-19. Iliwekwa mnamo 2010-01-28.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Dominic Monaghan kwenye Internet Movie Database
- Dominic Monaghan interview Archived 3 Machi 2007 at the Wayback Machine.