Lost

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lost

Nembo ya Lost
Aina Maigizo, Kutisha, Aksheni
Imeongozwa Jack Bender
Stephen Williams
na wengineo
Nchi inayotoka Marekani
Lugha Kiingereza
Ina misimu 5
Ina sehemu Oahu, Hawaii (Orodha ya sehemu)
Utayarishaji
Watayarishaji
wakuu
J. J. Abrams
Damon Lindelof
Bryan Burk
Jean Higgins
Jack Bender
Carlton Cuse
Edward Kitsis
Adam Horowitz
Elizabeth Sarnoff
Sehemu Oahu, Hawaii
Muda makisio ni dk. 43
Urushaji wa matangazo
Kituo ABC
Inarushwa na 22 Septemba 2002 - hadi leo
Viungo vya nje
Tovuti ya utayarishaji

Lost ni kipindi cha Marekani kinachohusu maisha ya watu waliopata ajali ya ndege iliyokuwa inatoka mjini Sydney, Australia na kuelekea mjini Los Angeles lakini ikaangukia na kupata ajali kwenye kisiwa kilichoko Oceania. Kipindi hiki kinaonyeshwa nchini Marekani kwenye stesheni ya ABC, na pia stesheni zingine kwenye nchi kadha.

Kwa ajili ya kuajiri waigizaji wengi, na kurekodi filamu mjini Oahu, Hawaii, kipindi hiki kinasemekana kuwa ni cha gharama ya juu sana kwenye historia ya filamu. Ilianzishwa na Damon Lindelof, J. J. Abrams na Jeffrey Lieber na imetayarishwa na ABC Studios, Bad Robot Productions na Grass Skirt Productions. Muziki wake umeundwa na Michael Giacchino.

Kipindi hiki kinachosifika kilivutia watazamaji milioni 16 kwenye mwaka wa kwanza. Imeshinda tuzo nyingi kama Primetime Emmy Award for Outstanding Drama Series mnamo 2005[1] na tuzo la Golden Globe Award for Best Television Series - Drama|Best Drama mnamo 2006.

Wahusika wakuu[hariri | hariri chanzo]

Kutoka kushoto kwenda kulia: Faraday, Boone, Miles, Walt, Michael, Ana Lucia, Charlotte, Ilana, Frank, Shannon, Desmond, Eko, Ben, John Locke, Kate, Jack, Sawyer, Sayid, Libby, Sun, Jin, Claire, Hurley, Juliet, Charlie, Nikki, Paulo, Richard, Rousseau, Bernard, Rose na Vincent
  • Naveen Andrews aliigiza kama Sayid Jarrah, ambaye ni askari wa kutoka nchi ya Iraq.
  • Emilie de Ravin aliigiza kama Claire Littleton, mwanamke mjamzito wa kutoka Australia.
  • Matthew Fox aliigiza kama Jack Shepherd, ambaye ni daktari.
  • Jorge Garcia aliigiza kama Hugo Reyes, ambaye ni mshindi wa pesa zilizomletea shida.
  • Josh Holloway aliigiza kama mwizi aitwaye James Ford.
  • Yunjin Kim aliigiza kama Sun-Hwa Kwon, ambaye ni mwana wa mwanabiashara maarufu.
  • Daniel Dae Kim aliigiza kama Jin-Soo Kwon, mumewe Sun.
  • Evangeline Lilly aliigiza kama Kate Austen, ambaye ni mfungwa.
  • Dominic Monaghan aliigiza kama Charlie Pace, ambaye ni mwimbaji maarufu na mtumiaji madawa ya kulevya.
  • Terry O'Quinn amaye aliigiza kama John Locke.

Misimu[hariri | hariri chanzo]

Msimu wa kwanza (2004-2005)[hariri | hariri chanzo]

Ilikuwa na vipindi 25 vilivyokuwa vikionyeshwa kila Jumatano saa mbili usiku nchini Marekani kuanzia 22 Septemba 2004. Inatueleza jinsi ndege ya Oceanic 815 ilivyopata ajali. Uhai wa waliopata ajali unahatarishwa na wanyama wa msituni, jinamizi lenye miujiza, na wenyeji wabaya wa kisiwa hiki wajulikanao kama "The Others". Wanakutana na mwanamke wa Kifaransa - Danielle Rousseau - ambaye amekwama kwa kisiwa hiki kwa muda wa miaka 16.

Msimu wa pili (2005-2006)[hariri | hariri chanzo]

Ina vipindi 24 vilivyoonyesha kila Jumatano saa tatu usiku nchini Marekani na Canasa kuanzia 21 Septemba 2005. Msimu huu unazingatia vita vya waathiriwa wa ajali ya ndege dhidi ya "The Others". Tunaelezewa chanzo cha ajali ya ndege ya Oceanic 815.

Msimu wa tatu (2006-2007)[hariri | hariri chanzo]

Ina vipindi 23 vilivyoonyeshwa kila Jumatano saa tatu usiku nchini Marekani na Canada kuanzia 4 Oktoba 2006. Vita bado vinaendelea. Hata hivyo, waathiriwa wa ajali ya ndege wanapata mawasiliano na kundi linalokuja kuwaokoa.

Msimu wa nne (2008)[hariri | hariri chanzo]

Ilikuwa na vipindi 14 tu. Inaonyesha jinsi waokoaji walivyofika kwenye kisiwa hicho. Watu sita wajulikanao kama "Oceanic Six" walipata fursa ya kutoka kwenye kisiwa hiki.

Msimu wa tano (2009)[hariri | hariri chanzo]

Ina vipindi 17 vilivyoonyeshwa kila Jumatano saa tatu jioni nchini Marekani na Canada kuanzia 21 Januari 2009. "Oceanic Six" wanaamua kurudi kwenye kisiwa kwa kutumia Ajira Airways Flight 316.

Msimu wa sita (2010)[hariri | hariri chanzo]

Ilitangazwa kuwa itaanza Jumanne, 2 Februari 2010.[2]

Tuzo[hariri | hariri chanzo]

(Kushoto hadi kulia): Jorge Garcia-aliyeshinda tuzo la ALMA, Daniel Dae Kim, Damon Lindelof aliyeshinda tuzo la Emmy, Carlton Cuse na Bryan Burk

Tuzo za Primetime Emmy Awards[hariri | hariri chanzo]

  • J. J. Abrams alituzwa kwa Outstanding Directing For A Drama Series mnamo 2005.
  • Mnamo 2007, Terry O'Quinn alishinda tuzo la Outstanding Supporting Actor – Drama Series[3]
  • Mnamo 2009, Michael Emerson alishinda tuzo la Outstanding Supporting Actor In A Drama Series

Tuzo za Creative Arts Emmy Awards[hariri | hariri chanzo]

  • Mnamo 2005, Michael Giacchino alishinda tuzo la Outstanding Music Composition For A Series (Dramatic Underscore).

Golden Globe Awards[hariri | hariri chanzo]

  • Mnamo 2006, Lost ilishinda tuzo la Best Television Series – Drama[4]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 58th Primetime Emmy Award Nominees and Winners - Emmys.tv
  2. Natalie Abrams. "ABC Sets Lost Premiere Date", TVGuide.com. Retrieved on 2010-01-25. Archived from the original on 2010-03-27. 
  3. "'Lost': Season 3 Episode Guide", Entertainment Weekly, 2008-02-14. Retrieved on 2008-03-03. Archived from the original on 2008-02-19. 
  4. "Golden Globe Nominations and Winners (2006)", Hollywood Foreign Press Association. Retrieved on 2008-03-02. Archived from the original on 2008-03-09.