Danièle Boni-Claverie

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Danièle Boni-Claverie
Jina la kuzaliwa Danièle Boni-Claverie
Alizaliwa 1942
Nchi Ivory Coast
Kazi yake Mwandishi wa habari

Danièle Boni-Claverie (alizaliwa mnamo mwaka 1942) ni mwandishi wa habari na mwanasiasa huko nchini Ivory Coast. Alihudumu serikalini katika baraza la mawaziri katika nchi hiyo na alikuwa mwanzilishi na rais wa Jumuiya ya Muungano wa serikali..[1]

Ni binti wa "Alphonse Boni" , alizaliwa Tiassalé. Alifanya kazi kama mwandishi wa habari, akiwa mhariri mkuu wa gazeti na kisha kuwa mkuu wa Radiodiffusion Television Ivoirienne (RTI)).[1][2][3]

Hapo awali alikuwa mwanachama wa "Democratic Party of Côte d'Ivoire - African Democratic Rally | Democratic Party ya Côte d'Ivoire",. Boni-Claverie aliwahi kuwa Waziri wa mawasiliano katika serikali iliyokuwa ikiongozwa na Daniel Kablan Duncan kutoka 1993 hadi 1999. Alihudumu kama waziri wa wanawake, familia na watoto katika serikali ya Gilbert Aké kutoka 2010 hadi 2011.[1][4]

Alikamatwa mnamo Oktoba 2016 baada ya kushiriki katika maandamano ya kuomba rasimu mpya ya katiba ya nchi hiyo iondolewe.[5]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]