Chlorini
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Chlorini |
|
|---|---|
| Jina la Elementi | Chlorini |
| Alama | Cl |
| Namba atomia | 17 |
| Mfululizo safu | Halojeni |
| Uzani atomia | 35.453 |
| Valensi | 1, 3, 5, 7 |
| Kiwango cha kuyeyuka | 171.6 K (−101.5 °C) |
| Kiwango cha kuchemka | 239.11 K (−34.04 °C) |
| Asilimia za ganda la dunia | 0.19 % |
| Hali maada | gesi |
Chlorini (tamka: klorini) ni elementi yenye namba atomia 17 katika mfumo radidia maana yake kiini atomia chake kina protoni 17. Uzani atomia ni 35.453 na alama yake Cl. Ni elementi ya pili katika safu ya halojeni.
Katika hali sanifu ni gesi yenye rangi njanokijani. Inamenyuka haraka na elementi nyingine na kwa wanyama pia watu ni sumu.
Inapatikana kwa wingi katika maji ya bahari kama sehemu ya chumvi ya kawaida NaCl na pia ndani ya humvi ya KCl.
Matumizi yake ni kusafisha maji au kung'arisha karatasi kiwandani. Imewahi kutumiwa kama sehemu ya silaha kama gesi ya sumu.
| Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Chlorini kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |