Chama cha Waandishi wa Kifeministi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Chama cha Waandishi wa Kifeministi lilikuwa shirika la Marekani la kutetea haki za wanawake kutoka Berkeley, California, lililoanzishwa na Mary Mackey, Adrienne Rich, Susan Griffin, Charlene Spretnak, na Valerie Miner.[1]

Kikundi hiki kilianzishwa mnamo 1978, kilijulikana kwa jarida lao la kitaifa. Walilenga kuongeza vuguvugu la utetezi wa haki za wanawake mwishoni mwa miaka ya 1970 kwa kuunda mtandao thabiti wa waandishi wa kike kuwasiliana na kusaidiana. Walikuza kazi za wanawake bila kujali umri wao, tabaka, rangi na upendeleo wa kijinsia. Shirika hili ilichapisha jarida hili mara tatu kwa mwaka kupitia huduma ya malipo ya kujisajili kwa wasomaji na kukidhi bei zao kwa wanawake wasio na ajira au wa kipato cha chini.[2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Love, Barbara J., ed. (2006). Feminists Who Changed America. Chicago, Illinois: University of Illinois Press. uk. 291.
  2. AAA. "Heresies PDF Archive : THE HERETICS" (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2023-12-24.