Benue (mto)
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Mto wa Benue | |
|---|---|
|
|
|
| Chanzo | Nyanda za juu za Adamawa katika Kamerun |
| Mdomo | Niger |
| Nchi za beseni ya mto | Kameruni na Nigeria |
| Urefu | 1,400 km |
| Kimo cha chanzo | 1,34 m kwa 7°40'N 13°15'E |
| Kiasi cha maji kinachotolewa mdomoni | 2,400 m³/s (wastani ya miaka ya 1980) |
| Eneo la beseni (km²) | ?? km² |
Mto Benue (Kifaransa: Bénoué) ni tawimto mkubwa wa mto Niger. Chanzo chake ni katika nyanda za juu za Kamerun hasa milima ya Adamawa. Katika sehemuy a kwanza ya mwendo wake unatelemka mita 600 kwa mwendo kali. Karibu na mji wa Garua unaungana na mto Mayo Kébi. Baada ya mwendo wa 350 km mto unatoka Kamerun na kuingia Nageria karibu na bandari ya Jimeta. Hapa mto una upana wa kilomita moja unaoweza kupanua wakati wa mvua. Baada ya Yola mto unapokea tawimto wake muhimu zaidi mto Gongola.
Katika Nigeria mto ni njia muhimu ya kubeba mizigo na mazao ya nchi kati ya pwani ya Atlantiki na sehemu za bara.
Inaishia katika mto Niger kwa mji wa Lokoja.
Viungo vya Nje [hariri]
Kuhusu hali ya mito nchini Kamerun Habari za beseni ya Niger pamoja na Benue