Awadeya Mahmoud

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

'

Awadeya Mahmoud
Mahmoud katika sherehe ya kupokea tuzo yake ya Wanawake wa Ujasiri.
Amezaliwa1963
Kazi yakeMwanaharakati


Awadeya Mahmoud (kwa Kiarabu عوضية محمود) ni Mwislamu kutoka mchi ya Sudan ambaye ni mwanzilishi na mwenyekiti wa Ushirika wa Wanawake Wauzaji wa Chakula na Chai pamoja na Ushirika wa Madhumuni Mengi ya Wanawake katika jimbo la Khartoum, Sudan.[1][2]Tarehe 28 Machi 2016, Idara ya Jimbo la Marekani ilimtangaza kuwa mmoja wa wapokeaji wa Tuzo ya Kimataifa ya Wanawake wenye Ujasiri kwa mwaka huo.[3]

Maisha yake[hariri | hariri chanzo]

Awadeya Mahmoud alizaliwa mwaka 1963 nchini Sudan, katika eneo la Kusini mwa Kordofan na baada ya mzozo familia yake ilihama hadi Khartoum. Alifunga ndoa na mwaka 1986 alianza biashara ya kuuza chai ili kujipatia kipato. Hii ilikuwa ni kazi ya chini lakini alihitaji kusaidia familia yake. Mwaka 1990 alianzisha ushirika ambao ulitoa msaada wa kisheria na usaidizi kwa wanachama wake[4]. Ushirika huo uliitwa gropu la wa Wauza Chakula na Chai.

Kupitia ofisi ya ushirika, njia ya kisheria ilifadhiliwa sasa ili kupambana na mamlaka walipokamata vifaa vya wanachama (hasa wanawake) kwa kuuza chai na chakula barabarani. Mambo hayakuenda vizuri na alilazimika kutumikia kifungo cha miaka minne gerezani baada ya yeye na wengine kuwa na madeni baada ya uwekezaji mbaya. Baada ya kutolewa kwake, aliendelea kusaidia wanawake na ushirika ulikuwa na wanachama 8,000 Khartoum. Shirika hilo lilianza kuwakilisha wanawake waliotawanywa na mzozo huko Darfur na Maeneo Mawili.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. https://web.archive.org/web/20160330080648/http://www.state.gov/s/gwi/programs/iwoc/2016/bio/index.htm Idara ya Jimbo la Marekani. Imehifadhiwa kutoka kwenye chanzo cha asili tarehe 30 Machi 2016. Imepatikana tarehe 30 Machi 2016.
  2. AfricaNews https://www.africanews.com/2016/04/29/sudan-s-tea-girl-empowers-women/ Habari za Afrika. Imehifadhiwa kutoka ya asili tarehe 30 Aprili 2016. Ilirejeshwa tarehe 11 Juni 2021.
  3. https://web.archive.org/web/20160503001127/http://nytlive.nytimes.com/womenintheworld/2016/03/29/state-department-honors-14-female-leaders-from-around-the-world-with-international-women-of-courage-awards/ New York Times. Imehifadhiwa kutoka ya asili tarehe 3 Mei 2016. Ilirejeshwa tarehe 30 Machi 2016.
  4. https://www.emirates247.com/lifestyle/tea-lady-s-journey-from-sudan-to-white-house-2016-04-29-1.628730 AFP, 29 Aprili 2016, Emirates 247. Ilirejeshwa 9 Julai 2016
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Awadeya Mahmoud kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.