Angavurugu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Matabaka ya angahewa

Angavurugu ni tabaka la chini kuliko yote ya angahewa ya Dunia. Ina asilimiia 80 za tungamo yote ya angahewa, na asilimia 99 za tungamo yote ya mvuke maji na vipulizaji. Matukio zaidi ya halihewa yanatokea katika tabaka hili.[1] Kimo cha angavurugu ni takribani km 15.

Istilahi "angavurugu" inatokana na "anga" + "vurugu", kwa sababu ya kuvurugavuruga kwa upepo, dhoruba, na kadhalika, iliyo tabia maalumu ya tabaka hilo la angahewa.

Tabaka lililoko juu ya angavurugu huitwa angatando. Mpaka kati ya matabaka hayo mawili huitwa mpakavurugu.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Troposphere". Concise Encyclopedia of Science & Technology. McGraw-Hill. 1984. It [the troposphere] contains about four-fifths of the mass of the whole atmosphere. 
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Angavurugu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.