Albatrosi
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Albatrosi | ||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
|
Albatrosi ni ndege wakubwa wa bahari katika familia Diomedeidae. Baina ya spishi hizi yuko ndege mwenye mabawa marefu kabisa kuliko ndege wote duniani. Albatrosi Mlizi ana mabawa ambayo pamoja yana urefu wa 310 cm kwa wastani na urefu kubwa kabisa uliopimwa ulikuwa 370 cm. Rangi zao zinatofautiana kutoka nyeupe na mabawa kijivu hafifu mpaka mwili wote kijivucheusi. Wana domo kubwa sana na ncha yenye umbo la kulabu. Mirija ya pua miwili inapitia pande zote mbili za domo.
Ndege hawa huenda mbali sana wakipuruka na wanaweza kuzunguka dunia. Hawapigi mabawa sana baada ya kuruka angani, lakini wananyiririka kwa mabawa yaliyonyooshwa. Huwakamata ngisi, samaki na gegereka na hula mizoga pia. Kwa kawaida albatrosi huyatengeneza matago yao kwa visiwa vya mbali visipokaa watu wala mamalia wengine. Kabla ya kujamiiana dume na jike hutenga dansi ya kanuni kaida. Jike hulitaga yai moja tu.
[hariri] Spishi za Afrika
- Diomedea amsterdamensis, Albatrosi wa Kisiwa Amsterdam (Amsterdam Albatross)
- Diomedea epomophora, Albatrosi Mfalme (Royal Albatross)
- Diomedea exulans, Albatrosi Mlizi (Wandering Albatross)
- Phoebetria fusca, Albatrosi Kijivucheusi (Sooty Albatros)
- Phoebetria palpebrata, Albatrosi Mgongo-kijivu (Light-mantled Albatros)
- Thalassarche bulleri, Albatrosi wa Buller (Buller's Albatross)
- Thalassarche cauta, Albatrosi Utosi-mweupe (Shy Albatross)
- Thalassarche chlororhynchos, Albatrosi Domo-njano (Yellow-nosed Albatross)
- Thalassarche chrysostoma, Albatrosi Kichwa-kijivu (Grey-headed Albatross)
- Thalassarche melanophrys , Albatrosi Nyushi-nyeusi Black-browed Albatross)
[hariri] Spishi za mabara mengine
- Phoebastria albatrus (Short-tailed Albatross)
- Phoebastria immutabilis (Laysan Albatross)
- Phoebastria irrorata (Waved Albatross)
- Phoebastria nigripes (Black-footed Albatross)
[hariri] Picha