Yvonne Nèvejean
Mandhari
Yvonne Feyerick Nèvejean (1900 – 1987) alikuwa mmoja wa viongozi wa shirika lililosaidia kuwaficha watoto wa Kiyahudi nchini Ubelgiji iliyokuwa ikikaliwa na Wanazi wakati wa Vita vya Pili vya Dunia.
Alikuwa na mchango mkubwa katika kuficha watoto takriban 4000, wengi wao walikuwa wa familia na taasisi za Kikatoliki. Baada ya vita aliheshimiwa ndani na nje ya Ubelgiji. Mnamo mwaka 1965, aliteuliwa kuwa Wema Kati ya Mataifa na Yad Vashem, Mamlaka ya Kumbukumbu ya Holocaust huko Yerusalemu, na mnamo mwaka 1996 stampu ilitolewa nchini Ubelgiji ikiwa na picha yake.[1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Yvonne Nèvejean – her activity to save Jews' lives during the Holocaust, at Yad Vashem website
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Yvonne Nèvejean kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |