Yuyun Ismawati

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

'Yuyun Ismawati'

Yuyun Ismawati (alizaliwa mnamo mwaka 1964) ni mhandisi wa mazingira nchini Indonesia. Ambae alikuwa akifanya kazi ya kubuni mifumo ya usambazaji wa maji katika miji na maeneo ya vijijini. Ismawati pia alishughulika kubuni mifumo ya usimamizi wa maji taka nakupelekea kutunukiwa Tuzo ya Mazingira ya Goldman mnamo mwaka 2009. [1]

Yuyun Ismawati ni Mshauri,Mwandamizi na mwanzilishi mwenza wa Taasisi ya BALIFOKUS, shirika la mazingira lenye makao yake Bali. Yuyun ana uzoefu mpana katika masuala ya usimamizi wa mazingira mijini, afya ya mazingira na usafi, pamoja na masuala ya hali ya hewa na sumu. [2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Yuyun Ismawati". Goldman Environmental Prize. Iliwekwa mnamo 1 May 2009.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. "Yuyun Ismawati". Project Southeast Asia (kwa en-US). 2012-12-22. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-05-17. Iliwekwa mnamo 2016-05-27.  More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)