Wikipedia:Kumzuia mchangiaji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Pendekezo (halijakubaliwa bado)[hariri chanzo]

  • Wakabidhi wana haki ya kumzuia mchangiaji kwa muda (masaa, siku, wiki, miezi, mwaka au milele) ama kwa wikipedia yetu yote au kwa kurasa maalum pekee.
  • Kwa kawaida tunahitaji kumweleza mtumiaji kwanza kuwa amefanya kosa kabla ya kumzuia. Asizuiliwe kama hajapata bado sanduku la kumkaribisha (humo tunampa nafasi ya kujifunza utaratibu), isipokuwa akionekana moja kwa moja amekuja kwa kusudi la kuleta fujo.
  • tumebana wachangiaji mara moja wakija kuondoa maudhui kwenye kurasa, kuingiza matusi, kuingiza matangazo ya biashara kwa kuificha katika matini. Hapa tupime uzito tukiamua kumbana kwa muda fulani. Wengine wanaleta matangazo yaliyo wazi kwa kutoelewa utaratibu. Kuondoa maudhui mara nyingi ni kosa la mchangiaji mpya, ni vema kumzuia kwa siku 1, 2 pekee na kumwonya (na kuendelea kumwangalia). Akirudia tuongeze muda.
  • Wanaoleta matusi au kuficha matangazo ya kibiashara wanaonyesha nia mbaya, hatuwahitaji, wanaweza kuzuiliwa kwa mwaka au milele.
  • kila mtumiaji aliyebanwa ana haki ya kulalamika: hapo lazima wakabidhi wengine waamue, si yule aliyetangulia kumzuia.
  • mkabidhi anapata uwezo wa kumzuia mtumiaji kama ameandikisha anwani ya baruapepe; hii ni lazima ili kurahisisha kumwandikia malalamiko.