Wikipedia:Kiswahili Wikipedia Challenge/Submissions/Boniface Muganda.
Rufaa kutoka kwa mwanzilishi wa Wikipedia, Jimmy Wales
Leo, mimi nakusihi ufanye mchango kusaidia Wikipedia.
Nilianzisha Wikipedia mnamo mwaka wa 2001, na kwa kipindi cha miaka minane iliyopita, nimeshangaa na kunyenyekea kuona mamia ya maelfu ya wanaojitolea kujiunga na mimi kujenga kamusi kubwa zaidi katika historia ya binadamu.
Wikipedia si tovuti ya kibiashara. Ni jumuiya ya uumbaji, iliyoandikwa na kufadhiliwa na watu kama wewe. Zaidi ya watu milioni 340 watumia Wikipedia kila mwezi - karibu theluthi ya dunia iliyounganishwa na mtandao. We u mmoja wa jamii hii yetu.
Nina imani kwetu sisi. Nina imani kuwa Wikipedia inaendelea kuwa bora. Hilo ndilo wazo zima. Mtu mmoja anaandika jambo, mwingine analiboresha kidogo tu, na linaendelea kuwa bora zaidi kadri ya muda unavyoendelea. Ukipata kwamba ni muhimu leo, tafakari ni kiasi gani tunchoaweza kuhitimu pamoja katika miaka 5, 10, 20 ijayo.
Wikipedia ni kuhusu uwezo wa watu kama sisi kufanya mambo ya ajabu. Watu kama sisi huandika Wikipedia, neno mojamoja kila wakati. Watu kama sisi ndio tunaofadhili Wikipedia. Ni uthibitisho wa uwezo wetu pamoja kuubadilisha ulimwengu.
Tunahitaji kuhifadhi mahala ambapo kazi hii muhimu inafanyika. Tunahitaji kuhifadhi Wikipedia. Tunataka kuiweka iwe ya bure bila malipo yoyote na hata ya bure ya bure katika matangazo. Tunataka kuitunza iwe wazi - unaweza kutumia habari katika Wikipedia kwa njia yoyote unayotaka. Tunataka kuitunza iendelee kukua - kueneza maarifa kila mahali, na kuuakaribisha ushiriki kutoka kwa kila mtu.
Wakfu wa Wikimedia ni muungano ambao si wa kutengeneza faida ulioanzishwa mwaka wa 2003 nia yake ikiwa kuendesha, kukua, kulea, na kulinda Wikipedia. Kwa kutumia dola milioni kumi kila mwaka na wafanyakaziwasiozidi 35, wakfu huu unaendesha tovuti tano bora inayosomwa ulimwenguni kwote. Nakuomba msaada wako ili tuweze kuendelea na kazi yetu.
Tafakari ulimwengu ambao kila mtu kwenye sayari ana uhuru kupata jumla ya maarifa ya binadamu wote. Huko ndiko tunakoelekea. Na kwa msaada wako, tutafika huko.
Asante sana kwa kutumia Wikipedia. Wewe ni mmoja wa hadithi hii: tafadhali fanya mchango wako leo.
Jimmy Wales.
Mwanzilishi, Wikipedia
|-
| Rufaa kutoka kwa mwanzilishi wa Wikipedia, Jimmy Wales || worked with Boniface Muganda alone. translated from en. {{http://wikimediafoundation.org/wiki/Appeal/en?utm_source=2009_Jimmy_Appeal3&utm_medium=sitenotice&utm_campaign=fundraiser2009&referrer=http%3A%2F%2Fen.wikipedia.org%2Fwiki%2FConstitution&target=Appeal}}