Nenda kwa yaliyomo

Wikipedia:Badilisha jina la mtumiaji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kila mtumiaji aliyejiandikisha anatumia jina lilelile kwa miradi yote ya Wikimedia. Unaruhusiwa kubadilisha jina unalotumia lakini hutakiwi kuchangia wakati mmoja kwa kutumia majina tofauti, yaani kupitia akaunti mbili.

Kwa habari za undani zaidi angalia hapa Wikipedia:Changing_username.

Kwa kubadilisha njia ya mtumiaji kuna njia mbili.

1) Njia nyepesi ni kuunda akaunti mpya, wakati ukiacha akaunti ya kwanza jinsi ilivyo na kutoitumia. Hii unaweza kufanya mara moja.

a) Kwenye akaunti ya zamani fungua ukurasa wa mtumiaji, weka alama za {{retired}} mwishoni au mwanzoni, hifadhi ukurasa.
b) logout.
c) anzisha akaunti mpya.
d) kama umetumia Maangalizi (watchlist), unaweza kuyahamisha kwa maelezo yafuatayo: Help:Copying_watchlist_to_new_username

Mbinu hii inapendekezwa hasa kama hujaunda bado makala nyingi na kuwa na michango mingi. Maana wengine hawatatambua kwa urahisi ukusiano kati ya jina la zamani (linalopumzika) na jina jipya.

2) Kwa kuomba msaada wa msimamizi mwenye madaraka ya kubadilisha majina (global renamer). Faida yake hapa ni kwamba utaona michango yako ya awali ukibofya kiungo cha "Michango" (kinaonyeshwa juu kabisa kwenye ukurasa wako, upande wa kulia). Makala zako za awali zitaonyeshwa kwa jina la awali lakini zinaunganishwa na ukurasa mpya. Anayetafuta jina lako la awali atapelekwa kwenye ukurasa wako mpya,

a) Fungua ukurasa wa Wikipedia:Changing_username/Simple, usome yote na kubofya sehemu ya "Click here to request a username change"

AU

b)Njia nyingine ni kufungua Special:GlobalRenameRequest na kuingiza jina unalotaka.