Wikichanzo:Ee Mungu Nguvu Yetu
Mandhari
> Mwanzo
< wikisource:National anthems
Kenya
[hariri chanzo]- Ee Mungu nguvu yetu
- Ilete baraka kwetu
- Haki iwe ngao na mlinzi
- Natukae na udugu
- Amani na uhuru
- Raha tupate na ustawi.
- Amkeni ndugu zetu
- Tufanye sote bidii
- Nasi tujitoe kwa nguvu
- Nchi yetu ya
- Kenya tunayoipenda
- Tuwe tayari kuilinda.
- Natujenge taifa letu
- Ee ndio wajibu wetu
- Kenya istahili heshima
- Tuungane mikono pamoja kazini
- Kila siku tuwe nashukrani.