Wichita Eagle
Wichita Eagle | |
---|---|
Jina la gazeti | Wichita Eagle |
Aina ya gazeti | Gazeti la kila siku |
Lilianzishwa | 1872 |
Eneo la kuchapishwa | Wichita, Kansas |
Nchi | Marekani |
Mwanzilishi | Marshall Murdock |
Mhariri | Sherry Chisenhall |
Mmiliki | Kampuni ya McClatchy |
Mchapishaji | Pam Siddall |
Makao Makuu ya kampuni | 825 E. Douglas Wichita, Kansas 67201 |
Nakala zinazosambazwa | *. 90,648 - Kila siku *. 149,230 - Jumapili [1] |
Tovuti | www.kansas.com |
The Wichita Eagle ni gazeti la kila siku linalochapishwa katika eneo la Wichita, Kansas, Marekani. Linamilikiwa na Kampuni ya McClatchy, kampuni hii huchapisha magazeti mengine 31 kama lile la The Kansas City Star. Hili ndilo gazeti kubwa kabisa katika Wichita , Kansas na maeneo yanayozunguka eneo hilo.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Gazeti la Eagle lilianzishwa na lilihaririwa na Marshall Murdock katika mwaka wa 1852. Gazeti shindani lake kuu,Beacon, lilizinduliwa katika Oktoba ya mwaka huo. Majarida haya mawili yalishindana kwa miaka 88 mpaka mwaka wa 1960 ndipo Eagle lilinunua gazeti la Beacon. Magazeti yote yaliendelea kuchapishwa , Eagle lilichapishwa asubuhi na Beacon lilichapishwa jioni. Katika mwaka wa 1973, kampuni ya uchapishaji ya Ridder Publications ilinunua magazeti yote mawili. Kampuni za magazeti za Ridder na Knight Newspapers ziliungana na kuunda Knight Ridder katika mwaka wa 1974, kampuni hii ikaunganisha magazeti hayo mawili kuwa The Wichita Eagle-Beacon katika mwaka wa 1980. Katika mwaka wa 1989, neno Beacon likatolewa na jina la gazeti likawa The Wichita Eagle.
Gazeti hili lilijijengea jina katika taifa zima chini ya uhariri wa W. Davis "Buzz" Merritt Jr..Buzz alikuwa mmojawapo wa wanachama wa Civic Journalism au Public Journalism (Uandishi wa Uraia/Umma) waliotetea maadili ya muungano huu. Muungano huu haswa ulisema kuwa waandishi wa habari na wasomaji si watazamaji katika michakato ya kisiasa na kijamii bali ni washiriki pia.Unaendelea na kuagiza wanahabari hawafai kuripoti habari tu ni kama hawana msimamo bali washiriki na watoe maoni yao. Harakati za Civic Journalism zilihusisha kuwataka wasomaji na wanajamii wawe washiriki. Muungano huu umekua polepole na bali na kuwa itikadi tu, Uandishi kwa Umma umekuwa ukitendeka katika magazeti.
The Wichita Eagle lilionekana kama ndilo lililokuwa kwenye mstari wa mbele wa harakati hizi. Kwa mfano, katika uchaguzi wa 1990, jarida hili liliandaa kura ya maoni kwa wakazi 500 ili kujua matakwa yao katika jimbo yalkuwa gani. Kisha, uchaguzi ulipokuwa ukiendelea, wanahabari wa gazeti hili walijaribu kuwauliza wagombea kuhusu hisia zao kuhusu masuala haya. Walichapisha toleo kila wiki likiorodhesha masuala na misimamo ya wagombea. Mgombea alipokataa kuchukua msimamo aliripotiwa pia. Njia hii ilikuwa tofauti sana na utaratibu wa zamani wa kuripoti kuhusu ukweli uliokuwa katika hotuba za wagombea. Kama matokeo ya hayo, watu waliopiga kura katika eneo msingi la usambazaji wa Eagle walikuwa wengi sana hasa asili mia 43.3 kuliko asilimia 31 katika maeneo mengine ya jimbo hilo.
Gazeti la Eagle likawa sehemu ya Kampuni ya McClatchy, Knight Ridder iliponunuliwa na McClatchy katika mwaka wa 2006.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- H. Craig Miner, Wichita: The Early Years, 1865-80 (University of Nebraska Press, 1 Oktoba 1982) (Out of Print) ISBN 0-8032-3077-X
- W. Davis Merritt, Knightfall: Knight Ridder and How the Erosion of Newspaper Journalism is Putting Democracy at Risk (Amacom Books, 30 Machi 2005) ISBN 0-8144-0854-0
- Michael Hoyt, (Julai 1992) "The Wichita Experiment", (Columbia Journalism Review)
- The McClatchy Company, Newspaper Profiles: The Wichita Eagle Ilihifadhiwa 12 Oktoba 2009 kwenye Wayback Machine..