Nenda kwa yaliyomo

Utofauti wa vizazi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Utofauti wa vizazi ni utofauti wa kimtizamo kati ya kizazi kimoja na kizazi kingine kiimani, kisiasa au kimatabaka. Kwa matumizi ya leo, utofauti wa vizazi unaonekana ni kati ya vijana na wazazi au wazee.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Kati ya wanasosholojia wa mwanzo kama Karl Mannheim aliona tofauti kwenye vizazi mbal mbali kwa namna vijana wanavyopitia ujana kwenye utuuzima akajifunza njia ambazo vizazi wanajitenga na vizazi vingine majumbani, makanisani, makundi ya watu wazima na makundi ya vijana.

Nadharia ya kisosholojia ya utofauti wa vizazi ilikuja kwa mara ya kwanza mwaka 1960 wakati vizazi vipya walikuwa wakienda tofauti na vitu vingi ambayo wazazi wao walikuwa wakiamini kwa nyanja mbalimbali kama muziki, siasa na utamaduni.

Kutenganisha utofauti wa vizazi

[hariri | hariri chanzo]

Kuna njia mbalimbali za kutofautisha vizazi. Kwa mfano majina wanayopewa makundi mbalimbali ya vizazi kama vizazi kimya, vizazi X, vizazi milenia na vizazi alfa na kila kizazi huwa na uvumi wao pamoja na athari katika jamii zao.

Matumizi ya lugha

[hariri | hariri chanzo]

Inaweza kutofautishwa kwa matumizi yao ya lugha. Utofauti wa vizazi umeleta utofauti kwenye lugha unaosababisha ugumu kuwasiliana. Tatizo hili limeonekana kwenye jamii na kusababisha mkinzano kwenye mawasiliano ya siku na siku, nyumbani, shuleni na kazini.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
  1. https://www.dictionary.com/browse/generation-gap
  2. https://books.google.com/books?id=FYElqUmQttgC