Umoja wa Vijana wa Umoja wa Mataifa
Umoja wa Vijana wa Umoja wa mataifa ni taasisi zisizo za kiserikali inazoongozwa na vijana wanaojitolea.
Malengo
[hariri | hariri chanzo]Lengo ni kuongeza nguvu katika kanuni za Umoja wa Mataifa kati ya watu wa wa nchi zao ili kuunda mtizamo mzuri wa umma kuhusu malengo ya Umoja wa Mataifa na hivyo kushawishi wanasiasa kufanya kazi zaidi kuelekea kuimarisha kanuni za Umoja wa Mataifa.
Umoja huu pia unafanya kazi moja kwa moja katika kushawishi viongozi wa sasa na wa baadaye wa nchi zao kuwekea mkazo kanuni za Umoja wa Mataifa. Hii inafanyika kwa njia ya kushawishi na kuelimisha viongozi wa sasa na wa baadaye.
Shughuli
[hariri | hariri chanzo]Umoja wa Vijana wa Umoja wa Mataifa unafanya kazi ili kufikia lengo kwa kufanya miradi ya aina mbalimbali:
- kuendesha kampeni za usambazaji habari ili kujulisha umma kuhusu mada zinazohusiana na Umoja wa Mataifa kama vile Malengo ya Maendeleo ya Milenia
- kuandaa midahalo inayohusu mada zinazohusiana na Umoja wa Mataifa mfano katika shule na vyuo vikuu
- Kufundisha juu ya kazi ya Umoja wa Mataifa na kanuni zake katika shule za sekondari
- kufanya mikutano inayofanana na ya Umoja wa Mataifa ambapo wanafunzi hufanya mazungumzo kama yale ya Umoja wa Mataifa kuhusu vitengo vya Umoja wa Mataifa.
Uanachama
[hariri | hariri chanzo]Taasis hizi za Umoja wa Vijana wa Umoja wa Mataifa, hujumuisha wanafunzi wa shule za sekondari, na nyingine hujumuisha wanafunzi wa vyuo vikuu na wakati mwingine wanafunzi wa sekondari na vyuo vikuu hufanya kazi pamoja.
Umoja huu huweka kigezo cha umri mbalimbali kwa ajili ya ushiriki katika taasis hiyo. Baadhi huweka miaka 25, wengine miaka 30 na wengine ili mradi tu uwe bado ni mwanafunzi wa chuo kikuu.
Ukubwa wa Umoja huu unotofautiana kati ya nchi moja na nyingine Katika baadhi ya nchi, Umoja wa vijana wa Umoja wa Mataifa wana wanachama wengi kwa sababu wao ni shirika mwamvuli wa matawi mbalimbali ndani ya nchi hiyo, kila moja likiwa na wanachama wapatao 15. Katika nchi nyingine, umoja huu hujumuisha kundi dogo tu la vijana.
Aina mbalimbali za taasisi za Umoja wa Vijana wa Umoja wa Mataifa
[hariri | hariri chanzo]Vijana wanaofanya kazi ya taasisi hii huchagua aina tofauti za muundo wa uongozi:
- Vijana wanaweza kuunda taasis inayojitegemea - Umoja wa Vijana wa Umoja wa Mataifa - ambalo hufanya kazi bila kutegemea "shirika mama" la nchi yao ambalo ni Shirikisho la vyama vya Umoja wa Mataifa Katika namna hizi, uhusiano kati ya Umoja wa vijana wa Umoja wa Mataifa na shirikisho la vyama vya Umoja wa Mataifa unachukua muundo tofauti yaweza kuwa kwa Umoja wa Vijana kuwa taasisi inayojitegemea na kufanya kazi katika ushirika na Shirikisho la vyama vya Umoja wa Mataifa au kwa msingi wa taasisi ya vijana kuwa na kiti katika bodi ya shirikisho la Umoja wa vyama vya umoja wa mataifa.
- Pia kuna Mashirikisho ya Vyama vya Umoja wa Mataifa ambayo hayan "Vijana" katika muundo wao lakini uongozi wake ukiwa umeundwa na vijana kwa kiasi kikubwa.
- Aidha, kuna sehemu ya Vijana ndani ya Shirikisho la umoja wa vyama vya Umoja wa Mataifa likakuwa kama shirika la vijana ndani ya taasisi ya watu wazima.
- Mwisho, kuna programu za vijana za shirikisho la umoja wa Mataifa ambazo huchukua muundo tofauti.
Shirikisho la Dunia la Vyama vya Umoja wa Mataifa-Vijana - mwavuli wa mashirika ya kimataifa ya Vijana wa Umoja wa Mataifa yote.
[hariri | hariri chanzo]Shirikisho la Dunia la Vyama vya Umoja wa Mataifa - Vijana (WFUNA-Youth) ni upande wa vijana wa Shirikisho la Vyama vya Umoja wa Mataifa (WFUNA) na hivyo ni shirika mwamvuli wa kimataifa wa wa Vyama vya Vijana wa Umoja wa Mataifa na programu zake kote duniani.
Ni taasisi isiyo ya kiserikali inayoongozwa na vijana na inayojumuisha kabisa vijana wanaojitolea.
Shirikisho la Dunia la Vyama vya Umoja wa Mataifa - Vijana linalenga kuongeza msisitizo wa kanuni za Umoja wa Mataifa kati ya umma na hasa vijana kwa kuimarisha shughuli za taasisi za Umoja wa Mataifa za Vijana na zile za upande wa vijana katika shirikisho la vyama vya Umoja wa Mataifa duniani kote. Shirikisho linataka kuhimiza uanzishwaji wa wa taasisi za Umoja wa Vijana wa Umoja wa Mataifa ambapo hazipo.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Shirikisho la Dunia la Vyama vya Umoja wa Mataifa - Vijana (WFUNA-Youth) Archived 13 Februari 2010 at the Wayback Machine.