Nenda kwa yaliyomo

Uhuru na Umoja (Marekani)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

"Uhuru na Umoja" ndiyo kauli mbiu rasmi ya jimbo la Marekani la Vermont. Kauli mbiu hiyo ilipitishwa kwa mara ya kwanza mnamo 1788 ili kutumika kwenye Muhuri Mkuu wa Jamhuri ya Vermont. Ira Allen alitengeneza muhuri wa Vermont na mara nyingi anajulikana kama mwandishi wake. Kitabu cha Allen cha 1798 The Natural and Political History of the State of Vermont kinataja michango mingi aliyotoa katika kuanzishwa kwa Vermont. Kufuatia kukubaliwa kwa Vermont katika muungano wa shirikisho mnamo 1791, bunge liliidhinisha tena matumizi ya kauli mbiu hio ya muhuri mpya wa serikali.

Gavana wa kwanza wa Vermont, Thomas Chittenden, alitoa kauli mbiu ya serikali katika nukuu yake: "Out of storm and manifold perils rose an enduring state, the home of freedom and unity." Akimaanisha kuwa kwenye dhoruba na hatari nyingi kuliibuka hali nzuri na amani,nyumba ya uhuru na umoja.[1]

Kuna makubaliano ya jumla kwamba kauli mbiu hio ya Vermont inahusu wazo la kusawazisha maadili mawili yanayoonekana kinyume: uhuru wa kibinafsi na uhuru wa raia mmoja mmoja, na manufaa ya pamoja ya jumuiya kubwa zaidi. Mwandishi na mkazi wa Vermont Dorothy Canfield Fisher (18791958) aliandika yafuatayo kuhusu hali yake ya kupitishwa: "wazo la Vermont linakabiliana kwa nguvu na tatizo la msingi la mwenendo wa binadamu - jinsi ya kupatanisha mahitaji ya kikundi, ambayo kila mwanamume au mwanamke mwanachama anapitia."

Nguvu hizi mbili zimestahimili zaidi katika historia ya Vermont, uhuru, na umoja, zikionyesha sehemu tofauti za utambulisho wa Vermont. Wito wa Vermont unaaminika kuwa msukumo wa hotuba maarufu ya Daniel Webster ya Uhuru na Muungano mbele ya Seneti ya Marekani. Matumizi ya kauli mbiu halisi hupatikana katika makundi mawili tofauti kabisa ya kisiasa. Chama cha mrengo wa kushoto cha kidemokrasia ya kijamii cha Ujerumani kilitumia kauli mbiu ya Uhuru na Umoja kabla ya Vita vya Pili vya Dunia.

Nchini Uingereza, chama cha mrengo wa kulia, chama cha kidemokrasia cha kingereza ambacho kinatafuta ulinzi wa utamaduni wa Kiingereza na kupinga umoja wa Ulaya, pia kinatumia kauli mbiu hii kikamilifu. Kauli mbiu ya sasa ya kitaifa ya Ujerumani, iliyopitishwa na Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani mnamo 1952, pia inafanana kabisa, kauli mbiu hii kwa kusema "Einigkeit und Recht und Freiheit" ikitafsiriwa kama "Umoja,Haki na Uhuru". Nembo ya jimbo la

Uswizi la Vaud inasomeka "Liberté et Patrie" - uhuru na nchi baba.

Matumizi

[hariri | hariri chanzo]

Kwa sheria ya Vermont kauli mbiu ya Uhuru na Umoja inatumika katika muhuri Mkuu, nembo, na bendera ya Vermont. Kauli mbiu hii inaweza kupatikana katika malango makuu ya Mahakama ya Juu ya Vermont, na juu ya jukwaa katika Ukumbi wa Wawakilishi katika Ikulu ya Vermont.

Tanzania

[hariri | hariri chanzo]

Kauli mbiu rasmi ya Tanzania ni msemo wa Kiswahili Uhuru na Umoja, unaotafsiriwa kama "Uhuru na Umoja".

  1. Webster's concise encyclopedia of flags & coats of arms. Internet Archive. New York : Crescent Books : Distributed by Crown Publishers. 1985. ISBN 978-0-517-49951-1.{{cite book}}: CS1 maint: others (link)