Uhifadhi wa maji
Uhifadhi wa maji unahusu kupunguza matumizi ya maji na kuchakata maji taka kwa malengo tofauti kama kusafisha, viwanda, kilimo nk
Maskani
[hariri | hariri chanzo]Teknolojia ya kuokoa maji ya nyumbani ni pamoja na:
- Vichwa vya mifereji ya kuoga vyenye viwango vya chini vya mtiririko(Low-flow shower heads) (wakati mwingine huitwa vichwa vyenye ufanisi wa kinishati kwani pia zinatumia nishati kidogo, kutokana na kiasi kidogo cha maji kuchemshwa). [onesha uthibitisho]
- Vyoo visivyohitaji nguvu nyingi kusafisha (Low-flush toilets) na vyoo vya kuhifadhi(composting toilets). Hivi vina makubwa katika ulimwengu uliyoendelea, kwani kwa kawaida vyoo vya Magharibi hutumia maji kwa wingi.
- Maji chumvi (maji ya bahari) au maji ya mvua yanaweza kutumika kwa kusafisha vyoo.
- Vipulizi vya faucet, ambayo huvunja mtiririko wa maji kuwa matone faini ili kudumisha "ufanisi wa unyevu" wakati huo ukitumia kiasi kidogo cha maji. Faida ya nyongeza ni kwamba zinapunguza kuruka kwa maji wakati wa kuosha mikono na kuosha sahani.
- Marudio ya matumizi ya maji taka (reuse)) au mifumo ya kuchakata, huruhusu:
- Marudio ya matumizi ya maji kwa kusafisha vyoo au bustani, na
- Usafishaji wa maji taka kupitia utakaso katika kituo cha kutibu maji. Angalia pia marudio ya matumizi ya maji taka
- Kuchota maji ya mvua
- Mashine za kusafisha nguo zenye ufanisi wa hali ya juu
- Vifaa vinavyosimamia unyunyi
- Midomo ya mifereji inayojifunga wakati haitumiwa, badala ya kuruhusu a hose kukimbia.
Maji pia inaweza kuhifadhiwa kwa kupanda mimea asili na kwa kubadilisha tabia, kama kufupisha muda bafuni na kutoachilia maji yakitiririka wakati unasafisha meno.
Kibiashara
[hariri | hariri chanzo]Vifaa vingi vya kuokoa maji (kama vyoo vya kusafishwa na maji kidogo) ambayo ni muhimu katika makaazi pia inaweza kufaa katika kuokoa maji katika biashara. Teknolojia zingine za kuokoa maji kibiashara ni pamoja na:
- Sehemu za mkojo zisizo na maji
- Usafishaji magari bila maji
- Faucet za Infrared au zinazoendeshwa na mguu- , ambazo zinaweza kuokoa maji kwa kutumia mitiririko fupi ya maji katika kuosha jikoni au bafuni
- Vifagiomaji vyenye presha, ambavyo vinaweza kutumika badala ya mifereji kusafisha mapito.
- Mifumo wa kurudia mizunguko ya kutengeneza filamu za X-ray
- Vifaa vya kusimamia uenezaji katika minara ya kupoesha
- Vifaa vya kuokoa maji ya mvuke, kwa matumizi ya hospitali, nk
Kilimo
[hariri | hariri chanzo]Kwa unyunyizaji wa mazao ufanisi wa juu kwa maji unamaanisha upunguzaji wa hasara kutokana na uvukizi, mtiririko au kumwagika kwa maji chini ya ardhi. Sahani ya Uvukizi inaweza kutumiwa kubaini kiasi cha maji ya kinachohitajika kunyunyiza ardhi. Unyunyizaji wa gharika, iliyo kongwe na aina ya kawaida, kwa mara nyingi sana hukosa usawa katika usambazaji, kwani sehemu ya shamba hupokea kiasi kinachozidi cha maji ili kutoa wingi wa kutosha kwa maeneo mengine. Unyunyizaji wa kutoka juu, unaotumia mzunguko wa katikati au mifereji inayosonga-upande, inatoa ruwaza sawa zaidi na usambazaji unaweza kudhibitiwa. Unyunyizaji wa drip(tone) ni ghali sana na hautumiwi sana, lakini unatoa matokeo bora katika kufikisha maji kwa mizizi ikiwa na hasara ndogo.
Kama vile kubadilisha mifumo ya unyunyizaji inaweza kuwa ghali kutekeleza, juhudi za uhifadhi mara nyingi hulenga kuongeza ufanisi wa mfumo uliopo. Hii ni pamoja na kutawanya ardhi iliyoshikamana, kujenga kingo za mitaro kuzuia mtiririko, na kutumia unyevu wa udongo na vifaa vya kuhisi mvua kuongezea ratiba ya unyunyizaji.[1]
- Mashimo, ambayo yanachota maji ya mvua inayotiririka na kuitumia kuongezea maji ya ardhini. Hii inasaidia katika malezi ya visima vya maji vya ardhini nk na hatimaye hupunguza mmomonyoko wa udongo unaosababishwa na maji inayotiririka.
- Upunguzaji wenye manufaa yoyote katika upotezaji wa maji, matumizi, au taka;
- Upunguzaji katika matumizi ya maji unawezekana kwa kutekeleza uhifadhi wa maji au hatua za kuongeza ufanisi wa maji; au,
- Mazoea ya usimamizi wa maji ambayo yanapunguza au kuboresha matumizi ya manufaa ya maji. Hatua ya uhifadhi wa maji ni tendo, mabadiliko ya kitabia, kifaa, teknolojia, au kuboreshwa kwa muundo au mchakato unaotekelezwa ili kupunguza hasara, taka, au matumizi ya maji. Ufanisi wa maji ni chombo cha uhifadhi wa maji. Inayopelekea ufanisi zaidi katika matumizi ya maji na hivyo kupunguza mahitaji ya maji. Thamani na ufanisi wa gharama ya hatua ya ufanisi wa maji lazima utathminiwe katika uhusiano wake na madhara yake kwa matumizi na gharama ya maliasili nyingine (kama nishati au kemikali).[2]
Ufanisi wa maji
[hariri | hariri chanzo]Ufanisi wa maji unaweza kuelezwa kama uhitimishaji wa kazi, mchakato, au matokeo na kiasi kidogo cha maji yakinifu, au kiashirio cha uhusiano kati ya kiasi cha maji kinachohitajika kwa kusudi maalumu na kiasi cha maji kinachotumika, kinachochukuliwa au kinachofikishwa.[2]
Lengo na Muundo wa Mtandao wa Chini Kabisa wa Maji
[hariri | hariri chanzo]Ufanisi kigharama wa mtandao wa maji ya chini ni mwongozo wa kiujumla kwa ajili ya kuhifadhi maji ambayo husaidia katika kuamua kiasi cha chini cha maji safi na shabaha ya maji taka katika mfumo wa viwanda au mijini kwa kuzingatia mpangilio wa usimamiaji wa maji yaani inaangazia mbinu zote za kuokoa maji. Mbinu hii inahakikisha kwamba taka kipindi cha kurudisha malipo kilichotamaniwa na aliyeunda kimeridhishwa kwa kutumia mbinu ya Systematic Hierarchial Approach for Resilient Process Screening (SHARPS).
Mbinu nyingine iliyoanzishwa kwa upeo wa kuokoa maji ni mbinu ya uchambuzi wa maji wa pinch. Hata hivyo, mbinu hii inalenga tu kuongeza maji safi na kupunguza maji taka kupitia marudio ya matumizi na uzalishaji upya.
Angalia Pia
[hariri | hariri chanzo]- Amri za Berlin Kuhusiana na Raslimali za Maji
- Biolojia ya uhifadhi
- Maadili ya uhifadhi
- Harakati za uhifadhi
- Ufanisi kigharama wa mtandao wa maji ya chini
- Unyunyizaji naksi
- Harakati za Ecolojia
- Ulinzi wa mazingira
- Uhifadhi wa Makaazi
- Uvukizi wa Sahani
- Upeo wa juu wa kiwango cha maji
- Kilimo endelevu
- Kipimo cha matumizi
- Uchambuzi wa kuteleza kwa maji
- Mita ya maji
- Upimaji wa maji
- Pinch ya maji
- Mpangilio wa usimamizi wa maji
- WaterSense
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ [1] ^ US EPA, "Maji Safi Kupitia Uhifadhi", Watumiaji wa Desturi za Kilimo
- ↑ 2.0 2.1 Vickers, Amy (2002). Water Use and Conservation. Amherst, MA: water plow Press. uk. 434. ISBN 1-931579-07-5.
Asili
[hariri | hariri chanzo]- Helmle, Samuel F., "Water Conservation Planning: Developing a Strategic Plan for Socially Acceptable Demand Cont Programs" (2005). Archived 20 Aprili 2010 at the Wayback Machine.Applied Research Projects. Archived 20 Aprili 2010 at the Wayback Machine. Chuo Kikuu cha Jimbo la Texas Karatasi ya 2.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Nakala ya Ufanisi wa Maji, Nakala ya Wataalam wa Uhifadhi wa Maji
- Njia Rahisi za kuhifadhi maji Nyumbani
- Kuhifadhi Maji ndani na Nje ya Nyumba Archived 6 Mei 2009 at the Wayback Machine.
- Ukame na Njia za Kuokoa maji Archived 2 Desemba 2008 at the Wayback Machine. kutoka Shirika la Msalaba Mwekundu la Uingereza
- Uhifadhi wa Maji ( eneo la mada ya WQIC) Archived 23 Oktoba 2009 at the Wayback Machine.
- Muungano kwa Ufanisi wa Maji (AWE)
- H2O Conserve Archived 8 Agosti 2019 at the Wayback Machine. Kihasibu cha Maji
- Water Conserve: Tovuti ya Uhifadhi wa Maji Archived 11 Desemba 2009 at the Wayback Machine.
- maji Archived 31 Desemba 2008 at the Wayback Machine. "Ukame"
- Blue Gold na Maude Barlow
- Maji-itumie vyema Archived 10 Januari 2010 at the Wayback Machine.