Ugaidi Kusini kwa Sahara
Ugaidi katika Afrika ni tatizo kubwa na kuenea haraka sana. Miaka ya hivi karibuni, ugaidi umekua na umesambaa katika Afrika na Afrika Mashariki. Baada ya, mashambulio ya tarehe kumi na moja mwezi wa tisa mwaka wa elfu mbili na moja (au 9/11), vita ilianza dhidi ya ugaidi. al Qaeda walienea silaha zao za ugaidi mpaka Afrika na sasa tunaweza kuona kwamba makundi ya kigaidi yameibuka. Tatizo la uchumi dhaifu kwa mahali pengi katika Afrika, imesababisha kuvutia watu kujiunga katika makundi ya kigaidi.
Ugaidi
[hariri | hariri chanzo]Ugaidi imekuwepo kwa muda mrefu lakini inaweza kuwa gumu sana kufafanua. Kwa mradi huu, nitatumia ufafanuzi kutoka Umoja wa Mataifa (UN) kutoka mwaka elfu moja mia tisa tisini na mbili: "Mbinu wasiwasi-msukumo wa mara kwa mara hatua vurugu, walioajiriwa na (nusu) clandestine mtu binafsi, kikundi au serikali watendaji, kwa sababu za idiosyncratic, jinai au kisiasa, ambapo - kwa kulinganisha na mauaji - malengo ya moja kwa moja ya vurugu si malengo kuu." Ugaidi ni ufanisi sana sasa kwa sababu ni rahisi kutumia kwa vita ya kigorila au mbinu mbalimbali za kijanja kwa namna isiyofanana. Na mifumo ya kimataifa kwa uchumi, jamii, na utamaduni sasa na utandawazi, ugaidi umekuwa tatatizo la dunia nzima. Takwimu kutoka Global Terrorism Database (GTD), imesema kwamba matukio ya ugaidi zaidi ya elfu sitini na mmoja yalilipotiwa na asasi zisizo za serikali kwamba ugaidi umewaua watu laki moja na elfu arobaini kutoka mwaka wa elfu mbili (2000) mpaka mwaka wa elfu mbili na kumi na nne (2014). Lakini, ugaidi umetumia vita kwa muda mrefu kabla ya sasa kutumia mbinu za kisasa. Watu wachache wanasema kwamba ugaidi ulianza katika karne ya kwanza baada ya Kristo au kabla, lakini ugaidi ulibadilika sana kutoka wakati huo.
Kwanza, ugaidi unalenga kutengeneza hofu na tishio kutoka umma na kawaida unakuwa na mafanikio katika hili. Vita imezuka, na sasa ugaidi ni sehemu muhimu sana ya vita. Ni rahisi kuliko vita vya jadi kwa jeshi dogo kutumia jeshi kubwa kama jeshi la Mmarekani au jeshi la Mrusi. Kwa hivyo, ni muhimu sana kuelewa sasa kuhusu ugaidi, lakini inaweza kuwa vigumu sana kueleza na kusoma.
Kwa utafiti huu, itazungumza kuhusu mifumo ya ugaidi, maeneo ambayo mifumo inapatikana (kama: kidini, kiuchumi, kisiasa, kijamii, kiutamaduni, nk.), viwango vya ugaidi (kama binafsi, serikali na jamii za kimataifa), njia zinazotumika kupigana na ugaidi, na maoni yangu katika jitihada za kuzuia. Na mfumo wa ubepari na Nchi za Magharibi katika Afrika, changamoto zimefika. Washindi na watu ambao kushindwa na mfumo huu wanapigana kwa haki, pesa, na nguvu. Maisha na mifumo ya Magharibi imetengeneza kukosekana kwa usawa na sasa watu wanataka kupiga ili kukubalika mfumo wa kisasa. Watu wengi wanatumia sababu ya kidini, kiuchumi, kisiasa, kijamii, na kiutamaduni kuhalalisha mbinu zao, lakini hatimaye watu wanataka nguvu na fedha kwanza. Ugaidi unashina kutoka ukosefu wa ajira na nafasi katika jamii, ukandamizaji wa serikali, uvamizi wa kijeshi kama jeshi la Marekani katika Iraq na kama jeshi la Ethiopia na Kenya katika Somalia, kubaguliwa, na vitu vingine. Watu maskini ni rahisi kuajiriwa kwa sababu watu wengi wanataka pesa na maisha bora na hawajui njia ya kupata utajiri na furaha yake. Makundi mengi ya magaidi wanatumia dini kuwavutia watu ambao wanasaidia sababu zao. Vijana ni rahisi hasa kuwavutia na makundi ya ugaidi wanajua hili. Bila elimu, ajira, na imani, watu wengi watafanya kitu chochote kupata pesa na utimizaji na kwa hivyo kikundi kama ISIS, al-Shabaab, Boko Haram, nakadhalika kinawalipa watu na kinawapa fursa kutolewa hasira na kukatisha tamaa zao.
Afrika ni rahisi sana kwa ugaidi kusambaza kwa sababu watu bila ajira na fursa hawana nafasi nyingine. Nchi kama Somalia, Nigeria, DRC, Libya, na nakadhalika zina uchumi bila utilivu na usalama na kwa hivyo, vikundi vya kigaidi vinaweza kuvutia wafuasi kupiga kwa haki zao. Watu Waafrika wanahitaji pesa zaidi na elimu zaidi na vikundi kama al-Shabaab, Boko Haram, Jahba Afrika Mashariki, al-Hijra, na vingine vinaonekana kuwasaidia watu kutoka Afrika bila imani.
Ugaidi unaweza kufanya kazi katika viwana vitatu: binafsi, serikali, na jamii za kimataifa. Afrika inazo sehemu tatu na nitazungumza kuhusu kila aina ya ugaidi katika insha hii. Kwa sababu ya aina tatu ya ugaidi, inaweza kuwa gumu kubaini nini ni ugaidi na nini si ugaidi, lakini tukitumia ufafanuzi kutoka Umoja wa Mataifa itakuwa rahisi kuelewa. Ni muhimu sana kueleza kwamba ugaidi haikuwa mbya kwa watu wote. Ugaidi unaweza kuwasaidia watu wengi na tunachofikiri ni ugaidi ni tofauti sana kutoka maoni ya watu wengine. Mada hii ni gumu zaidi inavyofikiriwa na watu wengi na si rahisi kuchagua yupi ni mzuri na yupi ni mbaya.
al-Shabaab
[hariri | hariri chanzo]Kwa Afrika Mashariki, rushwa, ukabila, mipaka wazi, na changamoto nyingi nyingine zimesaidia kutengeneza historia ya vurugu na vita. Afrika Mashariki ina watu wengi Waislam ambao wamechangia na ukuaji wa ugaidi kule mikoani na ukosefu wa amani. al-Shabaab ni kikundi kikubwa cha ugaidi kwa Afrika Mashariki na kinafanya kazi kule Somalia na kuenea mpaka Kenya. al-Shabaab kimetengenezwa na Aden Hashi Farah Ayro katika mwaka wa elfu mbili na sita (2006) .
Aden Hashi Farah Ayro alipata msaada, mtaji, na mawazo mengi kutoka vikundi vya kimataifa kama al Qaeda na kwa hivyo, al-Shabaab imepata mafanikio haraka sana. al-Shabaab kimechukua udhibiti wa mahali pengi kama mji mkuu wa Mogadishu. Kwa muda mrefu, Somalia haijawa na usalama au serikali nguvu na kwa hivyo, imekuwa rahisi sana kwa al-Shabaab kuenea. Katika mwaka wa elfu mbili na kumi na moja (2011), Moktar ali Zubeyr alikuwa kiongozi wa kikundi hicho na yeye ametumia vurugu kuwapiga watu ambao hawakukubaliana na yeye.
al-Shabaab kimewawaajiri Wamarekani kusaidia na shughuli yake kama Msomalia ambaye alipiga sokoni katika Nairobi, Kenya mwaka 2016. Kikundi cha al-Shabaab kinaamini kwamba ni muhimu sana kuanzisha nchi huru kutoka ushawishi wa Magharibi kama Osama bin Laden. Viongozi wengi wa al-Shabaab wamepiga au wamefanya kazi na al Qaeda, lakini bin Laden hakutambua al-Shabaab kama sehumu ya al Qaeda katika mwaka wa elfu mbili na kumi na mbili (2012) baada ya Moktar ali Zubey alijuu mpaka nguvu.
al-Shabaab wanavipiga vikundi vichache, kama African Union Mission katika Somalia (AMISOM), jeshi la Marekani, na Forces of the Federal Republic of Somalia (FFRS). Nchi ya Somalia imekosa utulivu na serikali halali kwa muda mrefu. Katika mwaka wa elfu moja mia tisa tisini na moja (1991), serikali ya Mohamed Siad Barre iliondoka na vita ilianza. Sasa, jeshi la AMISOM linawatumia wanajeshi kimsingi kutoka Kenya, Uganda, Burundi na pia Nigeria, Sierra Leone na Djibouti kutengeneza jeshi la elfu kumi na saba ya watu. Major General Fred Mugisha ameamuru AMISOM kutoka mwaka wa elfu mbili kumi na moja (2012) mpaka sasa na yeye anatoka Uganda. Maj. Gen. Mugisha anataka kutumia mikakati ya usalama na pia mikakati ya jeshi kuishindwa al-Shabaab. Yeye alisema katika mwaka wa elfu mbili kumi na moja (2011) kwamba : Tunahitaji msaada wa wote wa amani na upendo wa Wasomalia kutusaidia kurejesha amani na utulivu kwa mji. Tunawaomba raia ili kusaidia serikali yao na kujitenga na kukataa wahalifu.”
al-Shabaab kiliundwa kutoka mabaki ya Al-Itihaad Al-Islamiya (AIAI). Baada ya kuanguka ya serikali ya Somalia katika mwaka wa elfu moja mia tisa tisini na moja (1991), Al-Itihaad Al-Islamiya kiliunda kulazimisha sheria ya Uislam (“Shariah law”) , lakini Ethiopia ilitazama maendeleo ya Islamism, Wahhabism na Salafism kama tishio kubwa kwa sababu Ethiopia kimsingi ni nchi ya Kikristo. Jeshi la Ethiopia liliingia Somalia na liliharibu makundi ya Al-Itihaad Al-Islamiya na Muungano wa Mahakama za Kiislam (ICU) katika shughuli za mwaka wa elfu mbili na nne (2004) na elfu mbili na sita (2006). Vipande vilivyobaki vya makundi vilichanganya kutengeneza al-Shabaab au “vijana” na al-Shabaab kilikua kwa haraka sana. Katika mwaka wa elfu mbili na tisa (2009), Jeshi la Ethiopia liliondoka na wanachama wa al-Shabaab walipigana wenyewe kuhusu mawazo ya viongozi wawili.
Sheikh Aweys alitaka kuzingatia malengo ya nchi tu na Sheikh Moktar Ali Zubeyr (au Godane) alitaka kuenea kimataifa. Hatimaye, Godane alishinda na al-Shabaab kiliahidi utii mpaka al Qaeda mwaka wa elfu mbili na kumi na mbili (2012). Yeye alifariki mwaka wa elfu mbili na kumi na nne (2014) kutoka bomu na ndege zisizo kuwa na rubani Marekani, na sasa Abu Ubaidah au Ahmed Omar ni kiongozi wa al-Shabaab. Yeye anapenda kushambulia vituo vya tassisi zisizo za kiserikali (NGOs) na Umoja wa Mataifa na kuwaaajiri vijana kutoka Kenya na nchi zengine.
al-Shabaab inataka kutengeneza nchi ya Kiislam kutoka katika nchi za Somalia, Ethiopia, Kenya, na Djibouti. Wanachama wa al-Shabaab wanataka maisha bora zaidi na viongozi wa kikundi hicho wanatumia matumaini hayo kuwavutia watu wapya, lakini, ukabila unasababisha matatizo kwa kikundi. al-Shabaab inafanya kazi yake kama serikali kwa mikoa yao na kwa kweli inatoa muundo wa maeneo ya nchi. Inatumia Maktabatu Maaliya (Wizara ya Fedha) na Amniyaad na wapelelezi (polisi wa siri) kama serikali. al-Shabaab kina mahusiano na yenye nguvu katika nchi yao na wanatumia elimu, dini, na mamlaka ya serikali kuongeza udhibiti wao wa nchi.
Wanapata pesa kutoka raia wa Somalia. Ripoti ya Umoja wa Mataifa kutoka mwaka wa elfu mbili na kumi na moja (2011) ilisema kwamba al-Shabaab ilikusanya pesa zaidi ya dola milioni mia moja kutoka kodi ya uwanja wa ndege, bandari, kodi za kidini, na kodi nyingine. Kinapata pesa kutoka Wasomali ambao wanaishi katika nchi nyingine, kama Wasomali wengi ambao wanaishi katika jimbo la Minnesota, Marekani. Labda kama vile asilimia kumi na nne (14%) ya Wasomali wanaishi nje ya nchi. Watu hawa wanatuma pesa kwa al-Shabaab, lakini ni gumu sana kutuma bila ugunduzi wa serikali. Kwa shughuli za kijeshi, al-Shabaab inatumia polisi wa siri, Amniyaad, mara nyingi. Amniyaad inajua mambo mengi kuhusu uwezo wa akili, mikakati ya vita, na kinatumia habari kujisaidia na sababu zao. Kikundi kinatumia wanajeshi kutoka nchi za nje, kama Iraq na Afghanistan, kuboresha jeshi lao na uwezo wake. Kawaida, al-Shabaab hutumia IEDs (improvised explosive devices) na kujitoa mhanga kwa kushambulia maeneo ya watu wengi. Sasa, wao wanatumia wazo la jihadi kuwavutia watu wapya kujiunga na wao. Kwa mfano, wataalama wachache wanafikiri kwamba washambuliaji wachache kutoka shambulio la Soko la Westgate katika nchi ya Kenya walikuja kutoka Marekani. Pia, al-Shabaab ni hatari sana kwa sababu ina eneo zuri na karibu na mpaka wa Yemen na Mashariki ya Kati. Wao ni wapiganaji madhubuti sana na tunahitaji kuwaona wao kama vile ni watu hatari sana.
al-Shabaab huajiri na hutegemea kutangaza kuhusu maovu ya serikali na haja kuharibu majengo na watu wa serikali au hoteli za kitalii kutimiza malengo yao. Lakini katika Kenya, kikundi kinatumia mgawanyiko katika jamii kutengenza matatizo. Aghalabu, wanatumia mgawanyiko katikati ya Waislam na Wakristo na kuhamasisha umuhimu wa umoja wa Kiislamu. Waislam wa Kenya wanakabiliwa na ubaguzi na mara nyingi hawalindwi na serikali, kwa hivyo al-Shabaab kinatumia nafasi hii kuwaajiri vijana wengine. Wanasiasa wa Kenya wanazingatia michezo ya kisiasa na ukabila na wanasahau kuhusu vijana wengi na changamoto hii inakuwa mbaya zaidi kwa sababu wanasiasa hawawasaidii vijana maskini.
Majeshi ya Somalia na Marekani yamechagua kuwalenga walengwa wenye thamani ya juu ndani ya al-Shabaab (high value targets - HVTs) na yamewaua watu wengi mwaka huu. Jeshi la Marekani limewashambulia HVTs kabla ya tukio maarufu la “Black Hawk Down” au Vita ya Mogadishu katika Mwezi wa Kumi mwaka elfu moja mia tisa tisini na tatu (1993). Lakini kutoka mwaka wa elfu moja mia tisa tisini na tatu (1993) mpaka elfu mbili na saba (2007) Jeshi la Marekani halijatumia mbinu hii au halijaingilia katika Somalia mara nyingi kwa sababu ya kushindwa katika Mogadishu na vitu vingine. Jeshi la Somalia limefanya ufanisi katika kuwakamata HVTs na linaendela kuwatumia wao kuwapata na kuwaua viongozi wengine wa al-Shabaab. Hata hivyo, mbinu hii peke yake imekuwa haitoshi. Wapiganaji ngazi ya chini wanaendeleza shughuli kama kawaida, lakini viongozi wengi wamejificha.
Ni muhimu sana kuelewa dini ya Uislamu na kukuza uvumilivu na elimu kupiga na kuacha ugaidi. Rushwa na umaskini vinatengeneza changamoto nyingi na zaidi. Pia, tunahitaji kufanya kazi na jamii kubaguliwa, kuwafundisha watu (hasa vijana), na kuwachagua watu wachache tu kuwalenga na kufunga gerezani kwa sababu vurungu zinaeneza ujumbe wao. Watu wa Somalia na watu wa nchi nyingine kama Ethiopia, na Somalia wanahitaji kushirikiana pamoja kutengenza mjadala wa wazi na utullivu na usalama kwa mkoa mzima.
Boko Haram
[hariri | hariri chanzo]Boko Haram ni kikundi kingine kilichoanza kuwa maarafu na utekaji wa wasichana 234 katika mwaka wa elfu mbili kumi na nne (2014) kutoka mji wa Chibok, lakini kilikuwa kimeundwa mapema zaidi. Kikundi kiliundwa rasmi katika mwaka wa elfu mbili na mbili (2002), lakini mara ya kwanaza hakikutumia vurungu. Kikundi kilianza kutumia vurungu baada ya mfululizo wa migogoro na serikali ya Nigeria katika mwaka wa elfu mbili na tisa (2009). Pia, imani zao zilikuwepo kwa muda mrefu kabla ya kundi (kama 1970s).
Boko Haram iliundwa na imani ya Mohammed Marwa au Maitatsine. Yeye alikuwa mhubiri wa itikadi kali wa Kiislam katika 1970s na 1980s na yeye hakupenda serikali ya Nigeria sana na mfumo wa maisha ya Kimagharibi. Maitatsine na wafuasi wake walipigana na serikali katika mwaka wa elfu moja mia tisa na themanini (1980) katika mji wa Kano. Vita ya uraia ilianza na kikundi cha Maitatsine kilipigana na serikali. Watu elfu nne waliuawa na Maitatsine huyo alikuwa miongoni mwao, lakini imani yake iliendelea na watu waliendelea kupigana na serikali ya Nigeria. Nigeria imekuwa na matatizo na migawanyiko ya kidini na kikabila na watu walipigana kuhusu kushika dola na rasilimali. Watu wa Kaskazini kimsingi ni Waislam wa Hausa au Fulani. Vikundi vya kikabila na watu wa Kusini kimsingi ni Wakristo kutoka vikundi vya Igbo au Yoruba na makundi haya walipambana mara nyingi. Wilaya kadhaa ziliweka sheria ya Uislam na matatizo yameendelea.
Katika mwaka wa elfu mbili na mbili (2002) kikundi cha wakuu wa dini ya Kiislamu na kiongozi aliyeitwa Mohammed Yusuf katika Borno, Nigeria kilitengeneza kikundi cha “Boko Haram”. Yusuf alianzisha shule ya Kiislam kwa watu maskini na yeye alikuwa na imani nyingi kama Maitatsine. Kikundi cha Boko Haram kilitaka kutengeneza nchi ya Kiislamu pamoja na sehemu ya kusini ya nchi. Kuanza Yusuf na kikundi chake kilikuwa cha itikadi kali, lakini si cha vurugu. Katika mwaka wa elfu mbili na tisa (2009), watu wachache wa kikundi walikataa kuvua kofia ya pikipiki wakati walipokuwa wamepanda pikipiki na walipigana na polisi. Maandamano ya vurugu yalianza na watu mia nne walikufa. Mohammed Yusuf alikamatwa na alihojiwa, na hatimaye polisi waliamua yeye akiwa bila hukumu. Baada ya hatua hii, Boko Haram ilianza kufanya vurungu sana na kiongozi mpya anayeitwa Abubakar Shekau.
Abubakar Shekau ametumia vurungu sana kuhamasisha hofu na kueneza ujumbe wa kikundi chake. Boko Haram kinapenda kuendesha shughuli zao katika majimbo ya Borno, Yobe, na Adamawa kwa sababu kinajua eneo vizuri sana na watu wengi wanakuja kutoka kabila la Kanuri. Pia, kimepata mazoezi kutoka vikundi kama Al Qaeda na al-Shabaab. Kwa mfano, Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Rais wa Somalia, Jenerali Abdirahman Sheikh Issa Mohamed, alisema kwamba wapiganaji wa Boko Haram walihamia Somalia kujifunza mbinu ya kutengeneza silaha, kufanya mashambulizi ya kujitoa mhanga, kutumia vita kwa mbinu mbalimbali, na kadhalika kutoka mwaka wa elfu mbili na kumi (2010) mpaka mwaka wa elfu mbili na kumi na mblii (2012) kutoka al-Shabaab. Vikundi vinaendelea kuzungumza na kwa hivyo al-Shabaab na Boko Haram vinafanya vitendo tofauti sana kutoka al Qaeda na ISIS (makundi mama yao). Katika miaka ya hivi karibuni, Boko Haram kimewapoteza watu wengi katika vita na serikali na hakifanyi kulinda eneo lao na kwa hivyo kimeanza kutumia mbinu kama al-Shabaab mara kwa mara.
Boko Haram hupata pesa kutoka vitu vingi. Kwanza, kinakusanya kodi kutoka kwa watu katika majimbo ya kaskazini pa Nigeria. Kinapata pesa kutoka kwa watu wa Nigeria na nje ya nchi na vikundi vya nchi nyingine kama Al Qaeda, al-Shabaab, ISIS sasa, na vikundi vingine. Mara nyingi, Boko Haram inawaibia benki na inawakamata watu wengi. Watu wa nchi nyingine kama Ufaransa, inawatumia kwa ajili ya fidia, lakini watu wa Afrika (Nigeria kawaida) inawauza kwa biashara siri ya utumwa. Kwa mfano, Boka Haram iliwachukua na iliwauza wasichana wa shule kutoka mashambulizi ya Chibok. Pia, inatumia uharamia katika pwani ya Nigeria na kimevamia msingi wa kijeshi kupata silaha. Boko Haram inapata kipato kutoka soko haramu pia kama kuuza madawa ya kulevia. Kwa muda mrefu, kinapata fedha kutoka Al Qaeda. Mohammed Yusuf aliruka mpaka Saudi Arabia mara moja na wataalam wachache wanafikiri kwamba yeye na Osama Bin Laden walianza makubaliano. Lakini hivi karibuni, kikundi kiliahidi utii mpaka ISIS na kinapata fedha kutoka kikundi hiki.
Kwa sasa, majeshi ya Chad, Cameroon, Niger, na Nigeria yamekilazimisha kikundi cha Boko Haram kurejea nyuma mpaka Msitu wa Sambisa, lakini kikundi kinaendelea kuwa hatari. Boko Haram kinakuwa na watuhumiwa wanajeshi 9,000 na watoto 2,000 kifungoni. Kinaweza kuendelea na vita kwa mbinu mbalimbali bila changamoto nyingi na kina hifadhi kubwa ya fedha na silaha kutoka mashambulizi katika msingi wa kijeshi.
Suluhisho Yamkini kwa Ugaidi na Changamoto
[hariri | hariri chanzo]Ni muhimu sana kwa watu wengi kuelewa kwamba vikundi kama al-Shabaab na Boko Haram si vikundi vya kidini tu. Maeneo ambayo mifumo ya ugaidi inapatikana ni magumu na ni mengi. Vichocheo vya kidini, kiuchumi, kisiasa, kijamii, na kiutamaduni vinafanya kazi pamoja kutengeneza mazingira mazuri ya ugaidi. Kwa al-Shabaab na Boko Haram, nchi za Somalia na Nigeria zina changamoto na ajira kwa vijana kwa muda mrefu. Vijana wengi wanapigana katika vikundi hivi kwa sababu wao hawana fursa nyingine kupata pesa na kuboresha maisha yao.
Kwa Somalia, vita na ukosefu wa utulivu unatengeneza mazingira bila fursa kwa ajira ya watu wengi na watu wanataka fedha kwa familia zao. Wasomalia wengi hawalipendi jeshi la Ethiopia na wanataka uhuru kutoka Ethiopia na nchi nyingine katika mambo ya nchi ya Somalia. Migawanyo ya kidini kati ya watu wa Kristo wa Ethiopia na watu wa Islam wa Somalia yanatengeneza hisia hasi. Muendelezo wa vurugu na vita katika Somalia zimefanya kazi ya kutengeneza mazingira kwa kikundu kama al-Shabaab kuenea zaidi kuliko kitu kingine chochote.
Katika Nigeria, serikali imetumia fedha kutoka katika uwekezaji kutoka nchi nyingine, kodi, na aina nyingine za kipato kuwekeza zaidi huko kusini mwa nchi katika uchumi wa mafuta. Kaskazini mwa Nigeria kuna uchumi wa kilimo kwa muda mrefu, lakini wafanyabiashara na watu mbalimbali waligundua hifadhi kubwa ya mafuta katika 1950s na pamoja na ukuaji mkubwa wa sekta ya mafuta katika 1970s Nigeria iliamua kuzingatia katika sehemu hii ya uchumi. Kwa hivyo, utajiri wa nchi hiyo uko katika kusini mwa nchi. Watu wa kusini walikumbatia elimu ya Magharibi katika zama za ukoloni na sehumu hii ya nchi palikuwa na viwanda vingi haraka sana, lakini watu wa kaskazini hawakutaka elimu ya Magharibi na watu wa Ulaya hawakujali kuhusu sehumu hii pia. Kuna tofauti kubwa ya usawa wa mapato na mgawanyiko wa kikabila kwa watu wa kaskazini na kusini na kwa hivyo, usawa unaendelea kuongeza. Serikali inatumia fedha kuboresha miundombinu kusini kuliko kaskazini mwa nchi ya Nigeria kuhamasisha uwekezaji zaidi na hii iliendelea kuwa mbaya zaidi na tatizo tu. Mgawanyo wa utajir kati ya kusini na kaskazi ulilingana na mgawanyo na watu Wakristo na watu Waislam na migawanyo hii inasaidia Boko Haram kuwaajiri na kueneza ujumbe wao kuhusu mabaya ya ubepari na elimu ya Magharibi.
Viwango vyote vya ugaidi vinatumiwa katika dunia ya kisasa kwa sababu vita imebadilika. Ugaidi unaweza kutumia viwango vya binafsi, vya serikali, na vya jamii za kimataifa kupata fedha, kupiga, na kufanya kazi. Ni vigumu sana kufuatilia njia za pesa kutoka nchi nyingi na mipaka kuwa wazi inavisaidia vikundi vya ugaidi kuendelea na kazi zao bila kuingiliwa na serikali. Kwa hivyo, tunahitaji kufanya kazi pamoja na kuachana na jamii za kimataifa kupinga ugaidi.
Serikali ya Somalia imepigana vita ya kimwili na vita ya kiitikadi kuonyesha kwamba kikundi cha al-Shabaab si cha Kiislam au Kisomali. Ukosefu wa utulivu mara kwa mara umekisaidia kikundi cha al-Shabaab sana kuwaajiri vijana na kuenea zaidi. Watu wachache wanaamini kwamba vitendo vikali vya serikali na jeshi la Nigeria kwa Boko Haram vilikilazimisha kikundi kuwa vurungu zaidi. Hii inaweza kuwa kesi kwa al-Shabaab na jeshi la Ethiopia na ni muhimu sana kuelewa madhara ya uvamuzi wa jeshi bila njia nyingine ya kusaidia.
Kwa Nigeria, serikali inahitaji kuwekeza katika sekta za kilimo na viwanda vya nguo katika kaskazini yaa nchi. Kwa Somalia, kwanza ni muhimu sana kuimarisha amani na utulivu kwa nchi na Wasomali. Nchi zote mbili zinalazimisha kuwekeza katika mfumo wa elimu na miundombinu bila kuzingatia amani ya nchi. Serikali zinahitaji kutengeneza mipango kukuza imani ya Waislamu wenye mlengo wa wastani na mipango kupunguza mitizamo hasi ya mfumo wa elimu ya Magharibi kwa kutumia shule za Kiislamu. Pia, tunahitaji kutumia uongozi mzuri na utawala kama hundi na mizani, uchaguzi wa haki, na kuheshimu haki za binadamu. Nchi zinahitaji kutekeleza mipaka vizuri ili kukomesha mtiririko wa silaha, fedha, na wapiganaji wa nchi nyingine kuingia nchi nyingine kwa urahisi. Watu wa Somalia na Nigeria wanahitaji kushirikishwa kupitia jumuiya mbalimbali.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Agbiboa, D. E. (2013). Why Boko Haram exists: The relative deprivation perspective. African Conflict & Peacebuilding Review, 3(1), 144–157.
Amundsen, I. (2010). Good governance in Nigeria a study in political economy and donor support Norad report 17/2010 discussion. Norwegian Agency for Development Cooperation.
Asuelime, L. E., David, O. J., & Onapajo, H. (2015). Boko Haram: The Socio-economic Drivers.
Busari, S. (2016, February 26). Boko Haram training in Somalia: Security chief. Retrieved September 27, 2016, from http://www.cnn.com/2016/02/25/africa/boko-haram-al-shabaab-somalia/index.html
Chibok abductions in Nigeria: 'More than 230 seized' (2014, April 21). Retrieved October 15, 2016, from http://www.bbc.com/news/world-africa-27101714
Chothia, F. (2015, May 04). Who are Nigeria's Boko Haram Islamists? Retrieved October 06, 2016, from http://www.bbc.com/news/world-africa-13809501
Cutting Off the Head of al Shabaab. (2016, September 09). Retrieved September 15, 2016, from https://www.stratfor.com/analysis/cutting-head-al-shabaab
Dearden, L. (2016, April 08). Isis: New terrorist group Jahba East Africa pledges allegiance to 'Islamic State' in Somalia. Retrieved September 10, 2016, from http://www.independent.co.uk/news/world/africa/isis-new-terrorist-group-jahba-east-africa-pledges-allegiance-to-islamic-state-in-somalia-a6974476.html
Ford, J. (2014, June 06). The Origins of Boko Haram. Retrieved September 27, 2016, from http://nationalinterest.org/feature/the-origins-boko-haram-10609
Forest, J. J. F. (2012). Confronting the terrorism of Boko Haram in Nigeria. Florida: Joint Special Operations University.
Fulgence N (2015) War on Terrorism in Africa: A Challenge for Regional Intergration and Cooperation Organizations in Eastern and Western Africa. J Pol Sci Pub Aff S1:007. doi:10.4172/2332-0761.S1-007. http://www.esciencecentral.org/journals/war-on-terrorism-in-africa-a-challenge-for-regional-integration-and-cooperation-organizations-in-eastern-and-western-africa-2332-0761-1000S1-007.php?aid=60680
Gartenstein-Ross, D. (2009). The Strategic Challenge of Somalia's Al-Shabaab. Middle East Quarterly.
Guest, R. (2004). The Shackled continent: Africa’s past. Present and Future Oxford: Pan books.
Iaccino, L. (2015, May 05). Nigeria Boko Haram: Chibok girls 'married off and sold as slaves' says former detainee. Retrieved October 12, 2016, from http://www.ibtimes.co.uk/nigeria-boko-haram-former-detainee-says-insurgents-told-her-chibok-girls-married-off-sold-1499713
Kabbani, S. H. (n.d.). Understanding Islamic Law. Retrieved October 23, 2016, from http://islamicsupremecouncil.org/understanding-islam/legal-rulings/52-understanding-islamic-law.html
Kinnan, C. J., et al. (2011). Failed State 2030: Nigeria-a Case Study.
McCoy, T. (2014, June 06). This is how Boko Haram funds its evil. Retrieved October 20, 2016, from https://www.washingtonpost.com/news/morning-mix/wp/2014/06/06/this-is-how-boko-haram-funds-its-evil/
Mohammed, A. S. (2015, May 03). OpEd: The Root Causes of Terrorism and Solutions. Retrieved September 21, 2016, from http://sahanjournal.com/root-causes-terrorism-solutions/#.WCAiKOGLRo5 Ilihifadhiwa 5 Februari 2016 kwenye Wayback Machine.
Muller, E. N. (1985). Income inequality, regime repressiveness, and political violence. American Sociological Review, 50(1), 47–61.
Musa, A. O. (2012). Socio-economic incentives, new media and the Boko Haram campaign of violence in Northern Nigeria. Journal of African Media Studies, 4(1), 111–124.
Nigeria's Boko Haram 'got $3m ransom' to free hostages. (2013, April 27). Retrieved October 07, 2016, from http://www.bbc.com/news/world-africa-22320077
Pejic, I. (2016). Terror in East Africa: Al Shabaab. Retrieved October 07, 2016, from https://southfront.org/terror-in-east-africa-al-shabaab/ Ilihifadhiwa 22 Machi 2020 kwenye Wayback Machine.
Shinkman, P. D. (2013, September 24). FBI Investigating American Involvement in Kenya Mall Attack. Retrieved September 14, 2016, from http://www.usnews.com/news/articles/2013/09/24/fbi-investigating-american-involvement-in-kenya-mall-attack
Shinkman, P. D. (2013, September 30). What You Need to Know About Terrorism in East Africa. Retrieved September 11, 2016, from http://www.usnews.com/news/articles/2013/09/30/what-you-need-to-know-about-terrorism-in-east-africa
Shinn, D. H. (2003, Fall). Terrorism in East Africa and the Horn: An Overview. Retrieved September 10, 2016, from https://journals.lib.unb.ca/index.php/jcs/article/view/218/376
Somalia Profile - Timeline. (2016, March 01). Retrieved September 14, 2016, from http://www.bbc.com/news/world-africa-14094632
Stewart, F. (2002). Horizontal Inequalities: A neglected dimension of development. WIDER Annual Lectures 5. Helsinki: UNU/WORLD Institute for Development Economics Research.
TFG/AMISOM COMMENCE OPERATIONS TO SECURE FINAL SECTOR OF MOGADISHU - AMISOM. (2011). Retrieved September 15, 2016, from http://amisom-au.org/2011/10/tfg-amisom-commence-operations-to-secure-final-sector-of-mogadishu/
Who are Somalia's al-Shabab? (2015, April 03). Retrieved September 11, 2016, from http://www.bbc.com/news/world-africa-15336689
Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |