Uga sumaku

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Vumbi ya chuma juu ya karatasi inajipanga katika mistari maalumu kama sumaku iko chini ya karatasi hii. Mistari hii inaonyesha mielekeo ya uga sumaku

Uga sumaku (ing. magnetic field) ni nafasi karibu na sumaku au mkondo wa umeme ambamo kani inaathiri magimba ndani yake. Uga sumaku hauonekani kwa macho lakini unapimika.

Kipimo cha SI kwa kutaja nguvu ya uga sumaku ni Tesla lakini mara nyingi kipimo cha kale cha Gauss kinatumiwa pia. Nguvu ya ugasumaku inapungua kadri ya umbali na chanzo chake.