Uchaguzi wa Rais wa Marekani, 1956

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Uchaguzi wa Rais wa Marekani, mwaka wa 1956 ulikuwa wa 43 katika historia ya Marekani. Ukafanywa Jumanne tarehe 6 Novemba. Upande wa "Republican Party", Rais Dwight Eisenhower (pamoja na kaimu wake Richard Nixon) alimshinda mgombea wa "Democratic Party" Adlai Stevenson II (pamoja na kaimu wake Estes Kefauver).

Matokeo[hariri | hariri chanzo]

Eisenhower akapata kura 457, na Stevenson 73 wakati mchaguzi mmoja kutoka Alabama alimpigia kura Walter B. Jones badala ya Stevenson. Ramani yaonyesha kura kwa kila jimbo.