Tone Tangen Myrvoll
Tone Tangen Myrvoll (amezaliwa 12 Mei 1965) ni mwanariadha wa zamani wa kuteleza barafuni, mbio za kuelekea na mbio za masafa marefu kutoka Norway ambaye ni kiziwi..[1] Ameiwakilisha Norway katika mashindano ya msimu wa joto na baridi ya viziwi ya kiolimpiki kuanzia mwaka 1985 mpaka 2003 kwenye matukio saba tofauti.
Tone ameshindana katika Michezo ya Majira ya Joto ya Viziwi mwaka 1985 na 1989 na kushindana katika Michezo ya Majira ya Baridi ya Viziwi mwaka 1987, 1991, 1995, 1999 na 2003. Tone Tangen Myrvoll alianza awali kazi yake kama mwanariadha wa kuelekea kabla ya kufuata kazi yake katika kuteleza kwa nchi kavu. Anachukuliwa kama mwanariadha wa kuteleza kwa nchi kavu aliyefanikiwa zaidi katika historia ya Michezo ya Viziwi akiwa na jumla ya medali 15 ikijumuisha medali 11 za dhahabu. [2]
Pia ni mwanamichezo mwenye mafanikio nchini Norway kwa kuweza kufanikiwa kushinda kwenye mashindano ya kiolompiki ya viziwi.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Tone Tangen Myrvoll, Skisport365.com". skisport365.com. Iliwekwa mnamo 2019-08-28.
- ↑ "Most successful Deaflympic athletes of all time". www.deaflympics2017.org. Iliwekwa mnamo 2019-08-28.