Tiktok

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
ikon ya TikTok kwa maneno

Tiktok (huko China inajulikana kama Douyin; kwa Kichina: 抖音; pinyin: Dǒuyīn) ni mfumo wa utangazaji wa video fupi unaomilikiwa na kampuni ya Kichina ya ByteDance[1]. Huandaa na kutengeneza aina mbalimbali za video za watumiaji wake katika muundo wa video fupi zenye dhamira tofautitofauti kama vile mizaha, vichekesho, hila, ucheshi, kucheza na burudani[2] [3] kwa muda wa sekunde 15 hadi dakika 10.

Tiktok ni toleo la Douyin ambalo liliachiwa sokoni mnamo Septemba 2016. Tiktok ilizinduliwa mnamo 2017 kwa iOS na Android kwenye masoko nje ya China, hata hivyo, ilipatikana duniani kote baada tu ya kuunganishwa na huduma nyingine ya mitandao ya kijamii ya China, Musical.ly, tarehe 2 Agosti 2018.

TikTok na Douyin ni mifumo inayofanana kwa mtumiaji lakini hawana ufikiaji sawa kimaudhui. Pia huduma zao na programu husika zinapatikana kwenye soko. Bidhaa hizo ni sawa ijapokuwa sifa zake zinatofautiana. Douyin inajumuisha mfumo wa utafutaji wa ndani wa nyuso za watu kwenye video zao na vipengele vingine kama vile kununua,kuweka nafasi kwenye hoteli na kufanya hakiki zenye lebo ya kijiografia. Tangu kuzinduliwa mwaka2016, Tiktok and Douyin zilipata umaarufu kwa kasi karibu sehemu zote duniani.Tiktok ilipata zaidi ya wapakuaji billioni 2 duniani kote mwezi octoba 2020.Morning Consult iliorodhesha TikTok kama chapa ya tatu inayokua kwa kasi zaidi 2020, Baada tu ya Zoom na Peacock. Cloudflare iliorodhesha TikTok kama tovuti maarufu ya 2021 kuzidi Google.

Tiktok imesemekana kuwa chanzo cha athari za kisaikolojia kama vile uraibu pamoja na mabishano kuhusu maudhui yasiyofaa, taarifa potofu, udhibiti na faragha ya mtumiaji.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Douyin ilizinduliwa na ByteDance huko Beijing, China mnamo Septemba 2016, awali kwa jina A.me kabla ya kuwa Douyin (抖音) mnamo Desemba 2016. ByteDance ilipanga kueneza Douyin nje ya China. Mwanzilishi wa ByteDance, Zhang Yiming, alisema kuwa "China ni nyumbani yenye moja ya tano tu ya watumiaji wa mtandao duniani kote, Ikiwa hatutapanuka kwa kiwango cha kimataifa, tutapoteza kwa nne ya tanoya watumiaji wanaoangalia.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]